Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa, Bw. Steven Mhapa akisikiliza hoja za madiwani.
Kaimu mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa Bw. Patric Golwike akiwasikiliza madiwani wa Halmashauri yake.
Makamu mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa Bi. Ritha Mlagala akiwa katika kikao hicho cha baraza la madiwani.
Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa wakiwa katika baraza lao.
" Tunasikiliza kwa makini" Niwa baadhi ya watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa wakiwa katika baraza la madiwani.
Baadhi ya watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa wakisikiliza kikao cha baraza la madiwani.
IMEFAHAMIKA kuwa
changamoto kubwa inayodumaza uchumi katika Halmashauri ya Wilaya ya Iringa, ni
pamoja na viongozi kukwepa kulipa ushuru wa biashara, pamoja na
baadhi ya mawakala kuiba fedha katika vituo vya ushuru.
Hayo yamezungumzwa na
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa, katika kikao cha baraza la
madiwani mabapo amesema viongozi wa aina hiyo wanavunja sheria
za ulipaji kodi, kwa kutumia wadhfa walionao.
Aidha Mhapa amesema baadhi ya vituo vya mawakala ni kitovu cha wizi wa fedha za ushuru, na hivyo
kuwataka wataalamu wa Halmashauri kupanga mkakati wa namna ya kudhibiti hali
hiyo, pamoja na njia sahihi za kubinafsisha ukushanyaji wa ushuru, ili
kuwasaidia wananchi kwa kurudisha asilimia 20 ya vijiji
vinavyotoa mazao hayo.
Aidha madiwani hao wameitaka serikali
kuyahimiza mashirika na asas za kiraia zinazojihusisha na ugawaji wa mipira ya
kiume (Kondomu) kuzigawa pia na kondomu za kike ili kuwawezesha wanawake kuwa
na uhuru wa matumizi ya dhana hizo.
Bi. Vumilia Mwenda diwani wa tarafa ya Kiponzelo/Ifunda, amesema
ubaguzi unaofanywa katika kuzigawa kondomu hizo unawanyima haki wanawake
kuwa na maamuzi ya kutumia zana hizo.
Naye Bi. Ameria Galinoma diwani wa Kata ya Kalenga amesema
kuna haja kondomu hizo zote zikawekwa katika vyoo vyote vya nyumba za starehe,
kwani baadhi ya wananchi wanaona aibu kununua madukani.
0 comments:
Post a Comment