Pages

Home » » Kikwete ataka wanaouza dawa za serikali TZ wakamatwe

Kikwete ataka wanaouza dawa za serikali TZ wakamatwe



Rais Jakaya Kikwete wa Tanzania ameiagiza Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii ishirikiane na Bohari Kuu ya Dawa nchini humo (MSD) kuwasaka wanaouza dawa za Serikali katika maduka yao, ili wachukuliwe hatua za kisheria. Aidha, amewaonya wanaohujumu dawa hizo na kuwataka waache mchezo huo mara moja kwa kuwa hatawavumilia wala kuwaonea huruma pindi watakapokamatwa, kwa sababu wamekuwa chanzo cha wagonjwa kukosa dawa katika hospitali za serikali, hususan vijijini. Sambamba na hilo, Rais Kikwete ameahidi kwamba serikali yake itahakikisha hospitali za umma zinapata dawa pamoja na madaktari wa kutosha ili kuimarisha kiwango cha afya Tanzania. Takwimu zinaonyesha kuwa zaidi ya asilimia 20 ya dawa za serikali huchukuliwa kinyemela na madaktari na kisha kuuzwa kwenye maduka na kliniki zao binafsi.
Jika Anda menyukai Artikel di blog ini, Silahkan klik disini untuk berlangganan gratis via email, dengan begitu Anda akan mendapat kiriman artikel setiap ada artikel yang terbit di Creating Website

0 comments:

Post a Comment

 
Support : Greyson Salufu | Chimbuko Letu Inc | Chimbuko Letu Inc
Copyright © 2011. Mbwile Media - All Rights Reserved
Template Modify by Chimbuko Letu Inc
Proudly powered by Blogger