WAKAZI wa Kata ya Bashnet, Wilaya ya Babati, mkoani
Manyara wamelaani kitendo cha mkazi mmoja wa kata hiyo kuwaingilia mbuzi, na
wameitaka Serikali kumchukulia hatua kali za kisheria kijana huyo. Baadhi ya wakazi wa eneo hilo wakiwamo wafugaji wamesikitishwa
na kitendo hicho cha kijana huyo kuwaingilia mbuzi wao.
Wakazi hao wamesema kuwa, ni mara ya tano sasa kwa kijana huyo
kumuingilia mbuzi wa mkazi mmoja wa eneo hilo, kitendo ambacho ni kinyume na
mila na desturi huku wakidai kuwa ni tabia ya muda mrefu kwa kijana huyo
kuwaingilia mbuzi hasa nyakati za jioni na kuwa, akishafanya kitendo hicho
anahama eneo hilo kwenda kujificha vijiji vya mbali.
Wamesema kuwa, wamekuwa wakifanya jitihada mbalimbali kuhakikisha
anakamatwa ili afikishwe kwenye vyombo vya sheria. Hata hivyo, Mtendaji wa Kijiji cha
Bashnet, Omary Mwanditi amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema kuwa, kijana
huyo amekuwa na tabia ya kuwaingilia mbuzi.
0 comments:
Post a Comment