TAARIFA
KWA VYOMBO VYA HABARI
Imetolewa:
Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya Chama Cha Mapinduzi itafanya Mkutano wake wa
kawaida kuanzia tarehe 10 -11 /02/2013. Kikao hicho kitaongozwa na Mwenyekiti
wa Taifa wa CCM, Dr. Jakaya Mrisho Kikwete.
Wajumbe wa NEC wanatarajiwa kufika Mjini Dodoma leo tarehe 9/02/2013,kwa ajili ya kikao hicho.
Pamoja na mambo mengine kikao hichi kitatanguliwa na Semina ya siku mbili kwa Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa.
Lengo la Semina hii ni kuwaongezea Wajumbe uelewa kuhusu masuala ya Chama Cha Mapinduzi na Serikali yake hasa ikizingatiwa kwamba wengi wa Wajumbe ni wapya kufuatia Uchaguzi Mkuu wa CCM wa mwaka 2012.
Mada zitakazowasilishwa kwenye Semina ni pamoja na;
1. Nafasi na Wajibu wa Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa
2. Umuhimu wa Maadili kwa Viongozi na Watendaji wa Chama Cha Mapinduzi.
3. Mikakati ya kutekeleza maazimio ya Mkutano Mkuu wa Taifa wa nane wa CCM.
4. Mkakati wa kukuza ajira nchini.
Semina hii itafuatiwa na Mkutano rasmi wa Halmashauri Kuu ya Taifa ambao pamoja na mambo mengine utafanya Uchaguzi wa Wajumbe wa Kamati Kuu ya Chama Cha Mapinduzi.

Nape Moses Nnauye
KATIBU WA NEC – ITIKADI NA UENEZI
KATIBU WA NEC – ITIKADI NA UENEZI
0 comments:
Post a Comment