NA BASHIR NKOROMO
KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Abdulrahman Kinana anaondoka nchini leo Machi 10, 2013, kwenda Jamhuri wa Watu wa China kwa ziara ya kikazi ya siku kumi, kufuatia mwaliko wa Chama Cha Kikomunisti (CPC) cha nchi hiyo.
KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Abdulrahman Kinana anaondoka nchini leo Machi 10, 2013, kwenda Jamhuri wa Watu wa China kwa ziara ya kikazi ya siku kumi, kufuatia mwaliko wa Chama Cha Kikomunisti (CPC) cha nchi hiyo.
Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa
(NEC) , Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migiro amesema
leo kwamba katika ziara hiyo Kinana atakuwa na msafara wa watu 14,
ambao baadhi yao ni Wajumbe wa Kamati kuu ya CCM, Makatibu wakuu wa
Jumuia za Chama na Wenyeviti wa Chama wa mikoa.
Akizungumza leo katika Ofisi Ndogo
ya Makao Makuu ya CCM, jijini Dar es Salaam, Dk. Asha-Rose alisema,
Kinana na msafara wake wanatarajiwa kufika Guangzhou China keshokutwa,
Machi 12, 2012.
Alisema, ziara hiyo ambayo ni ya
kwanza nje ya nchi kwa Kinana tangu kuteuliwa kwake kuwa Katibu Mkuu wa
CCM, Oktoba, mwaka jana,
imeandaliwa na Chama Cha
Kimomunisti cha China kwa lengo la kupata fursa ya viongozi wa ngazi ya
juu wa vyama hivyo kubadilishana uzoefu katika nyanja mbalimbali za
kisiasa na kiuchumi kwa manufaa ya vyama na wananchi wa nchi Dk.
Asha-Rose alisema baada ya kuwasili Guangzhou, kinana na ujumbe wake
wakiwa na wenyeji wao wa Chama Cha Kikomunisti cha China watatembelea
maeneo mbalimbali ikiwemo jiji la Dong-guan, Shenchen, Chengdu, Machi
13-14, 2013, msafara utakwenda jiji la Chengdu, Sichuan, Nanchong na
kumalizia ziara hiyo katika jiji la Beijing ambako atawasili Machi 18,
2013.
Tanzania na China zimekuwa na
uhusiano wa siku nyingi katika maeneo mbalimbali yakiwemo ya kiuchumi,
kijamii, kisiasa na kiutamaduni na pia Chama Cha Mapinduzi (CCM) na
Chama Cha Kimkomunisti cha China (PCP) ambavyo ni vikongwe vimekuwa na
mahusiano ya kidiplomasia kwa miama mingi na uhusiani huo uanelezwa
kuendelea kukua na kuimarika siku hadi siku.Ushirikiano unaoonekana kuwa
wa kindugu wa nchi hizo za Tanzania na China uliasisiwa tangu enzi za
waliokuwa viongozi wa nchi hizo,
Hayati Baba wa Taifa Julius
Nyerere na Mao Tse Tung.Moja ya miradi inayotghibitisha uhusiano na
urafiki wa kindugu baina ya China ya Tanzania, ni mradi mkubwa wa ujenzi
wa Reli ya TAZARA na maradi wa TAZAMA, Mradi wa zana za Kilimo
Ubungo, mradi wa kiwanda cha Mang’ula na wa kiwanda cha nguo cha
urafiki.
0 comments:
Post a Comment