Mwanasiasa
mkongwe Mzee Kingunge Ngombale Mwiru akizindua kitabu historia ya
Hayati Sheikh Kaluta Amri Abedi katika hafla iliyofanyika leo kwenye
ukumbi wa Karimjee jijini Dares Salaam. Mwanasiasa
mkongwe Mzee Kingunge Ngombale Mwiru akisisitiza jambo wakati
uzinduzi wa kitabu historia ya Hayati Sheikh Kaluta Amri Abedi katika
hafla iliyofanyika leo kwenye ukumbi wa Karimjee jijini Dares
Salaam.Kushoto ni Balozi Mstaafu Job Lusinde na kulia ni Brigedia
Hashimu Mbita.
…………………………………………………………….
MWANASIASA mkongwe nchini Kingunge
Ngomble Mwilu amewataka Watanzani kuienzi Lugha ya Kiswahili kama
nyenzo itakayosaidia katika kukuza na kuleta maendeleo katika elimu
nchini.
Kingunge aliyasema hayo jijini
Dar es Salaam jana, wakati wa uzinduzi wa kitabu cha Historia ya Hayati
Sheikh Kaluta Amri Abed, kilichoandikwa na Mathias Eugen ambapo uzinduzi
huo uliandaliwa na familia ya Kaluta na baadhi ya wataalamu wa lugha
hiyo kutoka Bakita.
Alisema anathamini uzinduzi wa
kitabu hicho ambacho kimekusanya kazi mbalimbali zilizofanywa na Hayati
Kaluta wakati wa uhai wake.
Kingunge alisema kila Taifa
duniani ili liweze kupiga hatua mbalimbali za maendeleo ni lazima liwe
na lugha inayofahamika vizuri na raia wake ambapo kwa Tanzania rugha
rasmi ni Kiswahili.
“Lugha ni chombo cha msingi kwa
binadamu pia inatofautisha kati ya binadamu na viumbe vingine ambapo
kupitia lugha ndipo tunapokuza uwezo wa kufikiri kwani huwezi kukuza
uwezo wa kufikiri biala ya kuwa na lugha ya kueleweka”alisema Kingunge.
Aidha, aliwapongeza akina
Hayati Kaluta na wenzake kwa kuiheshimu lugha hiyo ambayo mara zote
imekuwa ikitumika katika kujenga umoja wa taifa hilo.
Aliwasa Watanzani kuacha tabia
ya kukifanya Kiswahili kuwa ni tatizo na baadala yake kuwandaliwe
mikakati ya lugha hiyo ili iwe ya kufundishia katika vyuo vikuu nchi
lengo likiwa kujenga uelewa mzuli wa lugha, inayozungumzwa hata kwenye
Umoja wa Mataifa (UN).
Miongoni mwa watu maarufu waliohudhuria katika uzinduzi huo ni pamoja na Balozi Job Lusinde, Suleiman Hega, Hashim Mbita na wengine ambapo wote, kila mmoja alisistiza matumizi ya lugha hiyo kwa ufasaha.
0 comments:
Post a Comment