Muheshimiwa
Waziri wa Maliasili na Utalii Kahasheki akikata utepe kuashiria
uzinduzi wa matembezi ya amani ya Tembo Duniani kupinga mauaji ya Tembo
hao.
Muheshimiwa
Waziri wa Maliasili na Utalii Kahasheki akionesha moja ya vibao ambavyo
vinawaonesha Tembo wakati wa Matembezi hayo ya amani.
Kutoka
kushoto ni Mrs. Tibaijuka akifuatiwa na Muheshimiwa Waziri wa Maliasili
na Utalii Kahasheki,Mwenyekiti wa Tanzania Association of Tours
Operators Willbert Chambulo, na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Muheshimiwa
Magesa Mulongo.
Baadhi ya Wanafunzi wakiwa katika Matembezi ya Siku ya Tembo Duniani
Mkurugenzi mkuu wa Hifadhi za Taifa nchini(TANAPA)Bw.Allan Kijazi(T shirt nyeupe)akisalimiana na maafisa wa Mamlaka ya Hifadhi ya Taifa ya Ngorongoro leo kwenye uwanja wa ndege wa Arusha wakati wakimsubiri Waziri wa Maliasili na Utalii,Balozi Khamis Kagasheki kuongoza maandamano ua kupiga vita ujangili wa Tembo nchini
Wadau wakiwa wa Mali Hai Arusha wakiwa katika picha ya pamoja |
Na Mwandishi Wetu,Arusha
Waziri wa
Maliasili na Utalii,Balozi Khamis Kagasheki amesema serikali ya Rais
Jakaya Kikwete haitakubali utalii ufie mikononi mwake kwa kuwaacha
majangili kutamba kwa kuwaua hovyo wanyama mbalimbali hasa Tembo kwenye
Hifadhi za taifa nchini.
Balozi
Kagasheki leo ameongoza maandamano makubwa ya wadau wanaopinga vitendo
nya ujangili vinavyohatarisha uwepo wa Tembo kwa mika 15 ijayo kama
hatua mahususi hazitachukuliawa.
"Sasa
hakutakuwa na suala la wanaharakati kutaka kesi ziharakishwe mahakamani
kwasababu maafisa wetu wakikutana na majangili huko porini mambo
yatakua yanaishia huko huko,"alisema Kagasheki
Akizungumza
katika hafla hiyo iliyofanyika kwenye viwanja vya AICC Kijenge
,Mwenyekiti wa taasisi iliyoandaa maandamano hayo ya Tanzania
Association of Tour Operetors(TATO)Willy Chambuso alisema kuna kila
sababu ya serikali ya Tanzania kuzungumza na serikali ya China ambako
kumeonakana ni soko la pembe za Ndovu
0 comments:
Post a Comment