Hali ya chanzo cha maji kilivyo kwa sasa licha ya kuwa ni msimu wa masika.
Mhandisi wa maji wa mradi wa kitaifa wa Wanging'ombe bwana Bakari Mbinga akipokea maelekezo kwa mkuu wa mkoa wa Njombe Capt.Mstaafu Asseri Msangi juu ya uendeshaji wa mradi huo.
Mkuu wa mkoa wa Njombe akizungumza na kutoa maagizo kwa katibu tawala mkoa wa Njombe Bi.Mgeni Baruani kufuatilia uundaji wa bodi ya mradi wa maji wa wanging'ombe na Mradi wa Tove Mtwango.[katika ni meneja wa mradi wa maji wa Kitaifa wa Wanging'ombe Eng. Bakari Mbinga].
Matenki chanzo mradi wa maji wa Kitaifa wa Wanging'ombe yakiwa yamekauka kutokana na kukatika miundombinu yake.
hiki ni chanzo cha maji hayo kilichopo kijiji cha Masaulwa wilayani Wanging'ombe mkoani Njombe.
Na.Mwandishi wetu.
Mkuu wa mkoa wa Njombe Kepten
Mstaafu Aseri Msangi, amemwagiza katibu tawala wa mkoa Njombe Mgeni Baruani
kufuatilia utendaji kazi wa mradi wa taifa wa Maji wa Mbukwa uliopo
wilayani Wanging’ombe pamoja na ule wa
Tove Mtwango uliopo wilayani Njombe ili kuangalia namna inavyotekeleza majukumu
yake kwa wananchi.
Mkuu huyo wa mkoa alitoa agizo
hilo baada ya kutembelea chanzo cha mradi wa maji wa Mbukwa, na kushtushwa na
taarifa ya Meneja wa mradi huo Mhandisi Bakari Mbinga, kwamba kwa sasa anafanya
kazi bila kutoa taarifa ya utendaji kazi kwenye bodi kutokana na kutokuwa na
bodi ya maji, licha ya kuwa anapaswa kuwajibika kwenye bodi hiyo na kwamba kwa sasa anawasilisha taarifa zake za kazi katika wizara
ya maji pekee.
Meneja wa mradi huo wa maji
Wanging’ombe taifa Kwa sasa amesema anapeleka taarifa wizarani pekee kwa kuwa
bado hakuna bodi ambayo anatakiwa kutoa taarifa za mradi .
Baada ya kupokea taarifa za mradi
huo kutoka kwa meneja, mkuu huyo wa mkoa alimwagiza katibu tawala wa mkoa wa
Njombe Mgeni Baruani kufuatilia mradi huo pamoja na ule wa Tove Mtwango ili
kuangalia namna inavyofanya kazi na kuwataka mameneja wa miradi hiyo kutoa
taarifa za utendaji wao katika halmashauri husika, na kuunda bodi haraka
iwezekanavyo.
Kutokana na hali hiyo aliomba
ufafanuzi juu ya mikakati ya kukarabati miundombinu hiyo kutoka kwa meneja wa
mradi, ambaye alisema walishaandika kuomba sh. 99 bilioni ili kujenga upya
miundombinu hiyo kwa ajili ya kuwezesha maji kuhifadhiwa kwenye matenki.
Katika hatua nyingine Msangi
aliwataka wahandisi wa miradi ya maji mkoani Njombe kuweka mita za maji kwa
watu binafsi wanaowaunganishia huduma ya maji ili kuepuka upotevu na utumiaji
wa maji ovyo.
“Katibu tawala fuatilia hii
miradi jinsi inavyofanya kazi, na uhakikishe wanaunda bodi haraka kwa sababu
haiwezekani mtu afanye kazi kwa uhuru anavyojiamria yeye bila mtu wa
kumdhibiti,” alisema Msangi na Kuongeza.
“Mameneja wa miradi hii lazima mtoe
taarifa za utendaji kazi wenu kwa halmashauri, maana haiwezekani taarifa
zipelekwe wizarani Dar Es Salaam pekee wakati wanaokunywa maji haya ni watu
wangu, na ndio maana serikali ikaamua kusogeza mamlaka kwenye halmashauri. ”
Alisema inashangaza kuona hata
mradi wa Tove Mtwango mpaka sasa hauna bodi ya maji tangu uzinduliwe na Rais
Jakaya Kikwete mwaka 2011.
Hata hivyo mkuu huyo wa mkoa
alishangaa kuona matenki ya maji ya mradi huo hayafanyi kazi kutokana na kuvunjika kwa miundombinu, na hivyo
kulazimika maji kuunganishwa moja kwa moja mpaka kwa watumiaji bila kuhifadhiwa
kwenye matenki na kutibiwa, jambo ambalo alisema ni hatari kwa afya za wananchi
kutokana na kunywa maji ambayo si safi na salama.
Kutokana na hali hiyo aliomba
ufafanuzi juu ya mikakati ya kukarabati miundombinu hiyo kutoka kwa meneja wa
mradi, ambaye alisema walishaandika kuomba sh. 99 bilioni ili kujenga upya miundombinu
hiyo kwa ajili ya kuwezesha maji kuhifadhiwa kwenye matenki.
Katika hatua nyingine Msangi
aliwataka wahandisi wa miradi ya maji mkoani Njombe kuweka mita za maji kwa
watu binafsi wanaowaunganishia huduma ya maji ili kuepuka upotevu na utumiaji
wa maji ovyo.
0 comments:
Post a Comment