• LILITAKIWA KUMWAGILIA EKARI 400, SASA LAHITAJI MAMILIONI MENGINE
Na Daniel Mbega
MIAKA minne iliyopita, yaani mwaka 2009,
wakati ujenzi wa Bwawa la Maji katika Kijiji cha Magulilwa wilayani
Iringa unakamilika, wananchi wa kijiji hicho na Kata yote ya Magulilwa
waliamini walikuwa wamekombolewa.
Hiyo ilitokana na ukweli kwamba, mradi
huo ungetosheleza kilimo cha umwagiliaji cha hekta 400 pamoja na huduma
nyingine za kijamii likiwemo josho la kuogeshea mifugo kijijini hapo.
Hata hivyo, kwa miaka minne sasa, ndoto
hizo zimeyeyuka kwani bwawa hilo limeshindwa kufanya kazi baada ya
kujengwa chini ya kiwango licha ya kugharimu Sh 47 milioni, fedha ambazo
zilitoka kwenye Mradi Shirikishi wa Maendeleo ya Kilimo na Uwezeshaji
(PADEP – Participatory Agricultural Development and Empowerment
Project), Halmashauri ya Wilaya pamoja na nguvu ya wananchi.
Mradi wa bwawa hilo ndio uliokuwa pekee
kwa Mkoa wa Iringa kati ya miradi 69 ya malambo na visima iliyofadhiliwa
na Padep nchi nzima tangu mwaka 2004 ambapo hadi mwaka 2007 yalikuwa
yamegharimu jumla ya Sh 3,003,785,439.
Mikoa mingine na idadi ya malambo ikiwa kwenye mabano ni Arusha (5), Kilimanjaro (1), Manyara (28), Tabora (2) na Singida (32).
“Usimamizi mbovu ndio uliofanya bwawa
hili lijengwe kienyeji na chini ya kiwango licha ya kutumia fedha
nyingi, lakini hili ndilo lingekuwa mkombozi mkubwa wa wananchi wa
Magulilwa kiuchumi kwa sababu kuna eneo kubwa la bonde kwa ajili ya
kilimo cha umwagiliaji,” anasema Ernest Kasike, Diwani wa Kata ya
Magulilwa.
0 comments:
Post a Comment