Waislamu Jijini
Dar es salaam wamefanya maandamo yenye lengo la kushinikiza kiongozi wao kupewa
dhamana mahakamani licha ya maandamano hayo kupingwa na Serikali.
Kutokana na
maandamano hayo jeshi la polisi kanda maalumu ya Dar es salaam imelazimika
kutumia mabomu ya machozi kuwatawanya waumini hao wa dini ya kiislamu
walioonekana kuzagaa katika maeneo ya jiji hilo wakifanya maandamano.
Awali kabla
ya kufanyika kwa maandamano hayo Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam SADICK MECK SADIC alikutana na
viongozi wa dini hiyo na kukubaliana kutofanyika kwa maandamano hayo.
Hata hivyo
waislamu hao wameonekana kukaidi agizo hilo na
hivyo kuingia barabarani mara baada ya kumaliza ibada yao ya Ijumaa.
Kwa habari
zaidi kuhusu vurugu za huko jijini Dar
es salaam tutaendelea kuwafahamisha kupitia vipindi
vyetu vijavyo.
0 comments:
Post a Comment