Waziri wa Mambo ya Nje wa Rwanda
amesema kuwa nchi yake inakusudia kuwasilisha mashtaka yake kwa Katibu
Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusiana na ripoti ya umoja huo inayodai kuwa
Kigali inawasaidia waasi wa mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya
Kongo.
Louise Mushikiwabo amesema kuwa, ripoti ya Umoja wa Mataifa inayoituhumu Rwanda kuwa inawaunga mkono waasi wa Kongo ni pungufu.
Ujumbe wa Wataalamu wa Umoja wa Mataifa
unazituhumu Rwanda na Uganda kuwa zinawaunga mkono waasi wa Kongo ambao
hivi sasa wanadhibiti maeneo ya mashariki mwa nchi hiyo kubwa ya
katikati mwa Afrika.
Kundi hilo la wataalamu wa Baraza la
Usalama la Umoja wa Mataifa linasema kuwa, licha ya Rwanda na Uganda
kukanusha vikali madai hayo lakini hadi hivi sasa zinaendelea kuwaunga
mkono waasi wa M23 wanaoendesha mapigano dhidi ya serikali ya Kinshasa
hasa katika mikoa ya Kivu Kaskazini na Kivu Kusini ya mashariki mwa
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
0 comments:
Post a Comment