Serikali imetishia kuwatimua wawekezaji wa kampuni
ya madini ya Tanzanite one iliyopo Mererani wilayani Simanjiro iwapo
watashindwa kulipa deni la zaidi ya dola za kimarekani milioni 2.2 zilizotokana
na ukwepaji kodi .
Katibu mkuu Wizara ya
Nishati na Madini Eliakim Maswi ametangaza msimamo wa serikali wa kupitia upya
mikataba ya makampuni ya madini hapa nchini baada ya kugundulika kuwa yapo
makampuni kadhaa yamekuwa yakiendesha shughuli zake za madini bila kulipa
ushuru wa serikali kinyume cha sheria.
Akizungumza na chama cha
wanunuzi na wauzaji wa madini nchini TAMIDA,jijini Arusha jana,Maswi alisema
kuwa kampuni ya Tanzanite one imekuwa ikikwepa kulipa kodi ya mrahaba wa madini
tangu mwaka 2004 hadi 2008 na kufikia kiasi cha shilingi bilioni 3.4 fedha za
kitanzania.
Amesema kuwa kampuni
hiyo ilikuwa ikitumia ujanja wa kukwepa kulipa mrabaha wa mauzo pale
inapokuta soko la madini nje ya nchi limeongezeka na kwamba serikali kupitia
kitengo cha ukaguzi wa madini iliweza kubaini ukwepaji huo wa kodi na kuiamuru
kampuni hiyo kulipa kiasi hicho cha fedha au ifungashe virago.
Ameongeza kuwa iwapo
kampuni hiyo ingegoma kulipa deni hilo serikali ilikuwa tayari kuwatimua na
kuwamilikisha wazawa mgodi huo.
Kwa mujibu wa kamishina
wa madini kanda ya kaskazini Benjamin Mchwampaka alisema kuwa tayari kampuni
hiyo imeshaanza kulipa deni hilo na kwamba hadi sasa imeshatoa
malipo ya dola 200,000 zaidi ya fedha za kitanzania milioni 310,huku serikali
ikiitaka kuhakikisha inamaliza kulipa deni hilo hadi kufikia jamuari mwaka
2013.
Hata hivyo katibu huyo
ameitaka TAMIDA kuisaidia serikali kuyafichua makampuni yanayokwepa
kulipa ushuru wa madini wakiwemo baadhi ya wafanyabiashara wakubwa ili
wachukuliwe hatua na kusisitiza kuwa kwa sasa serikali imeanza mkakati wa
kupitia upya mikataba ya makampuni ya madini hapa nchini.
0 comments:
Post a Comment