WAKATI Uchaguzi wa Umoja wa Wanawake
Tanzania (UWT) umemalizika juzi, huku ukidaiwa kugubikwa na ubabe na rushwa,
Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) umejitapa kwamba, utahakikisha vitendo hivyo
havitokei katika uchaguzi wake mkuu utakaofanyika kuanzia leo mjini Dodoma.
UVCCM imeapa kwamba mgombea au hata
mpambe atakayebainika kujihusisha na kampeni zilizo nje ya utaratibu na kanuni
za UVCCM au kujihusisha na vitendo vya rushwa atashughulikiwa mara moja ikiwemo
kuchukuliwa hatua za kisheria.
Akizungumza na waandishi wa habari
mjini Dodoma, Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa CCM,Martine Shigela alisema,
wameweka mtandao mpana wa kutosha kukabiliana na aina yoyote ya ukiukwaji wa
tararibu, kanuni na sheria za uchaguzi wa UVCCM.
Shigela alisema, taratibu za mkutano
mkuu utakaoambatana na uchaguzi huo, zimekamilika na utafanyika kwenye ukumbi
wa Mwalimu Nyerere, uliopo Chuo Cha Mipango ambako ndiko ulikofanyika pia ule
wa UWT.
Amesema, mkutano unaanza leo, Oktoba
23, na utafunguliwa na Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete.
Katika nafasi ya Mwenyekiti
wanachuana wagombea watatu, Lulu Mushamu Abdallah, Sadifu Juma Khamis na
Rashid Simai Msaraka wakati katika nafasi ya Makamu Mwenyekiti ni Ally Salum
Hapi, Paul Christian Makonda Mboni Mohamed Mhita.
Nafasi zingine ni, Halmashauri Kuu
ya Taifa Viti sita (Bara) wagombea 40, Viti Vinne (Zanzibar) wagombea 22,
Nafasi ya Baraza Kuu la Vijana Taifa Viti vitano Bara wagombea 39 na viti
vitano Zanzibar wagombea 14, Uwakilishi Wazazi Taifa na Jumuia ya
Wanawake Tanzania (UWT) wagombea 16 kila nafasi.
0 comments:
Post a Comment