Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya Chama Cha Mapinduzi (CCM),Sambwee Shitambala
Na Thobias Mwanakatwe
Mjumbe wa
Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya Chama Cha Mapinduzi (CCM),Sambwee
Shitambala, amekitaka Chama cha Demokrasi na Maendeleo (Chadema) kuacha
siasa za kunung’unika pale wapinzani wao wanapowazidi.
Ametoa kauli hiyo jana wakati akizungumza na NIPASHE kwa njia ya simu kufuatia Katibu wa Chadema Mkoa wa Mbeya, Boid Mwabulanga, kueleza kuwa safu mpya ya uongozi iliyochaguliwa katika mkoa huo ni dhaifu hivyo itakiwezesha chama chake kuongeza majimbo zaidi katika uchaguzi mkuu wa 2015.
Hata hivyo, Shitambala ambaye ni mjumbe wa NEC kupitia Wilaya ya Mbeya Mjini, akijibu madai hayo alisema kauli ya Katibu huyo wa Chadema ni ya kutapatapa ambayo inaonyesha chama hicho kimeanza kuingia uwoga kutokana na kuchaguliwa viongozi makini ambao wataizika Chadema mkoani humo.
“Namshangaa Mwabulanga kuzungumza mambo hayo wakati tunafahamu mambo mengi yake tukianza kuyalipua atahama mji, mfano tunafahamu yeye ni kibaraka wa Katibu Mkuu wa Chadema, Dk.Willbroad Slaa, ambapo amepewa cheo hicho baada ya kuondolewa aliyekuwa Katibu wa Chadema, Eddo Makatta aliyechaguliwa kidemokrasi ndani ya chama hicho na siyo yeye (Mwabulamba) ambaye amewekwa tu kufanya kazi ya mtu,” alisema Shitambala.
Shitamba ambaye kabla ya kujiunga CCM alikuwa Mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa Mbeya, alisema alitegemea mtu ambaye ni kibaraka wa mtu fulani akapata ujasiri wa kusimama na kuponda uongozi wa CCM uliochaguliwa kidemokrasia tofauti na yeye ambaye amewekwa kwa maslahi ya mtu.
Kuhusu madai kwamba Chadema wataongeza majimbo katika mkoa huo, Shitambala alisema hizo ni ndoto kwa sababu viongozi waliochaguliwa ndani ya CCM wamejipanga kumaliza upinzani mkoani humo ikiwemo kurejesha majimbo ya Mbeya mjini na Mbozi Magharibi ambayo yanaongozwa na wabunge wa Chadema.
“Mwabulanga anasema Chadema wataongeza majimbo 2015, namfananisha na mpita njia aliyeokota pochi njiani ambaye atapenda kupita njia hiyo kila wakati akiwa na matumaini kwamba ataokota pochi tena,” alisema Shitambala akimaanisha makosa yaliyofanywa na CCM katika uchaguzi mkuu uliopita kamwe hayawezi kurudiwa.
Alisema CCM itahakikisha inapitisha majina ya wagombea udiwani na ubunge ambao wapo makini wanaokubalika na wananchi kwani makosa yaliyofanyika chaguzi zilizopita hayawezi kurudiwa na kupelekea majimbo kupotea.

CHANZO:
NIPASHE JUMAPILI
0 comments:
Post a Comment