Mtaalamu
wa Elimu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto –UNICEF
Zubeida Tumbo-Masabo akitoa ufafanuzi kuhusiana na umuhimu wa kuwa na
sera madhubuti za elimu zitakazopelekea kuboresha kiwango cha elimu
kuanzia ngazi za chini hadi za juu.
Na.Mwandishi wetu
Serikali
ya Tanzania imeshauriwa kuwa na sera ya mpya ya elimu kwa kuwa sera
iliyopo imepitwa na wakati na inasababisha mikanganyiko.
Mtaalamu
wa Elimu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto –UNICEF
Zubeida Tumbo-Masabo amesema upo umuhimu wa kuharakisha kutoa sera mpya
ya elimu kwa sababu ndio itakayorahisisha utekelezaji badala ya
kutokuwepo na sera inayo eleweka.
Aidha
amesema sera zilizopo sasa zimepitwa na wakati, hivyo sera
zitakazobuniwa upya zinapaswa kuwa na malengo ya kuendeleza elimu kwa
watoto haswa motto wa kike.
Bi.
Zubeida Tumbo-Masabo amesema vitendo vinavyofanyika sasa vya kumfukuza
shule mtoto wa kike kwa mfano aliyebakwa na kupata ujauzito ni kumtia
kitanzi cha maisha.
Ametumia
fursa hiyo kuelezea kuwa katika sekta ya Elimu Umoja wa Mataifa
unafanya shughuli za kuboresha elimu kitaifa, lakini pia inafanya kazi
katika ngazi ya wilaya maalum katika kuangalia yale mambo ambayo
wanayatilia mkazo na kuyachangia iwapo yamefanikiwa.
Katika
wilaya hizo Umoja wa Mataifa unafanya vitu mbali mbali ambapo kama
UNICEF imejikita katika kuangalia Masuala ya Upangaji Mipango, kwa kuwa
mara nyingi shule nyingi hazina mipango.
Bi.
Zubeida Tumbo-Masabo amefafanua kuwa shule zinapokuwa na mipango
thabiti zinaweza hata kuuza mipango hiyo kwa mashirika mengine na
kujipatia fedha za kuendesha shughuli zao nyingine za hapo shuleni.
0 comments:
Post a Comment