Ndege kama hii zikiwa mbili zimeonekana kwenye anga la jiji la Mbeya huku zikipita kwa kasi wakazi wa jiji la Mbeya waingiwa na hofu kubwa wakidhani ndio mambo ya Malawi yameivaaaaa............!Si unajua kuwa kwa muda kumekuwa na uvumi wa nchi hizi mbili kuingia kwenye vita ya mpaka wa ziwa nyasa
Meneja wa viwanja vya Ndege Mbeya EZEKIEL MWALUTENDE ameuambia mtandao huu kuwa kinachofanyika sasa ni mazoezi ya ndege kwenye uwanja huo ana kusema kuwa pamoja na ndege za kivita pia zipo ndege za abiria 5 ambapo zoezi hilo linatarajia kukamilika Jumanne wiki ijayo.
Ndege
ya kwanza kutua katika Uwanja Wa Ndege Wa Kimataifa Wa Songwe mkoani
Mbeya Jumapili Julai 22 2012, ilikuwa ndege aina ya Forker 28 ambayo
alikuwemo Rais Jakaya Kikwete na msafara wa watu wengine 31.
Uwanja huo ambao aujakamilika na kudaiwa kuwa matengenezo yake yamefikia asilimia 95 tu bado aujaanza kutumika rasmi.
Baada
ya kutua kwenye uwanja huo majira ya saa tano na dk 15 , rubani wa
ndege hiyo, Kapteni Dominick Boman, akiongozwa na Meneja wa Uwanja wa
ndege wa Mbeya ilipotua, Valentine Kadeha, aliusifia kuwa una sifa zote
za kurusha ndege kubwa zinazobeba abiria na kuhoji kwa nini haujaanza
kutumika.
“Uwanja
ni mzuri sana, sehemu ya kurukia ndege ni pana na uwanja ni mrefu
hakika wananchi wana kila sababu ya kuufurahia, sijui kipi kinakwamisha
kuanza kutumika kwa abiria labda vituo vya mafuta havijajengwa, suala la
sehemu ya kushukia abiria si tatizo; marubani tunahitaji uwanja mzuri,”
alisema Bomani.
Mkurugenzi wa Mamlaka ya Viwanja vya ndege, Suleiman Suleiman, alisema uwanja huo utaanza kutumika rasmi Novemba Mosi.
0 comments:
Post a Comment