Na
Venance Matinya,
MWANAMKE
anayetuhumiwa kumnyanyasa mtoto wa dada yake kwa kumfungia ndani na kumchoma
kwa maji ya moto, hatimaye amepandishwa kizimbani leo katika mahakama ya Wilaya ya
Mbeya kujibu shtaka linalomkabili.
Mwendesha
mashtaka wa Serikali, Achiles Mulisa ameiambia Mahakama kuwa Mtuhumiwa Wilvina
Mkandala (24) alitenda kosa la kusababisha majeraha akiwa na nia ovu ambayo
imemsababishia ulemavu mtoto Aneth.
Mulisa
akisoma mashtaka hayo mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi wa mahakama hiyo Gilbert
Ndeuruo amesema kosa hilo ni kinyume cha kanuni ya adhabu kifungu cha 222(a) sura ya 16 kama ilivyorejewa mwaka
2002.
Kutokana
na kosa hilo mshtakiwa amekana shitaka hilo ambapo amerudishwa mahabusu hadi
Novemba 22, Mwaka huu kesi hiyo itakapotajwa tena.
Mwendesha
mashtaka huyo alisema Mshakiwa amenyimwa dhamana kutokana na hali ya mhanga
ambaye ni mtoto Aneth kutokuwa ya kuridhisha na kuongeza kuwa sababu nyingine
ni kwa ajili ya usalama wake.
Alisema
upande wa Jamhuri unamashahidi wanne ambao wataanza kutoa ushahidi wake
mahakamani hapo Novemba 22, Mwaka huu kutokana na upelezi kukamilika.
Aliwataja
mashahidi hao kuwa ni Mwenyekiti wa Mtaa wa Majengo Shukuru Mwakanyamale,
Daktari anayemtibu mhanga katika Hospitali ya Rufaa ya Mbeya Dr. Paul.
Wengine
ni Askari Polisi aliyepeleleza kesi hiyo WP Pudensia na Habiba Mwakanyamale ambao
wako tayari kufika mahakamani na kutoa ushahidi wao mbele ya mahakama.
Awali
mshatakiwa huyo aliieleza mahakama kuwa na uhusiano na mtoto huyo ambapo pia alikiri kuwa na taarifa za
kile kinachoendelea juu ya matibabu ya mtoto huyo na kuhusu kukatwa kwa mkono
wake wa kushoto na kufungwa bandeji ngumu(POP) kwenye mkono uliobaki.
0 comments:
Post a Comment