Paroko |
Paroko msaidizi |
Mbali na kupigwa risasi katika ubavu wake wa kushoto na kujeruhiwa vibaya katika tukio hilo lililotokea majira ya 4.45 usiku wa kuamkia leo, Padri Burgeo alijeruhiwa vibaya nyuma ya kichwa chake baada ya kupigwa na nondo.
Akizungumza na wanahabari katika hospitali ya mkoa wa Iringa ambako viongozi wamelazwa kwa ajili ya matobabu, Kaimu Mganga Mfawidhi wa Hospitali hiyo, Dk Faustine Gwanchele alisema Padri Myalla amejeruhiwa vibaya kichwani baada ya kupigwa kwa panga na nondo.
"Walifikishwa majira ya saa sita usiku wa kuamkia jana, na wakaanza kupatiwa matiababu wanayoendelea nayo mpaka sasa," alisema na kuongeza kwamba Padri Bergeo alianza kufanyiwa upasuaji jana ili kuondoa vipande vya risasi vilivyopo ndani ya mwili wake.
Dk Gwanchelle alisema hali ya Nzigilwa ni mbaya kwasababu majambazi waliomjeruhi walimvunja mfupa wa sehemu ya nyuma ya kichwa chake.
Kwa hisani ya lukwangule blog Tanzania
0 comments:
Post a Comment