Katika hali isiyokuwa ya kawaida mtu mmoja aliyejulikana kwa jina
la Tumsifu Mwambusi (20),mkazi na mkulima wa Kijiji cha Mwela,Wilaya ya Rungwe
Mkoani Mbeya amefumaniwa akimbaka ng’ombe.
Tukio hilo la ajabu yake limetokea mwaka
huu majira ya saa mbili za usiku ambapo jamaa huyo alikwenda kwenye makazi ya
Bwana Leonard Mwangwemba,kisha kuingia ndani ya zizi na kuanza kumbaka
ng’ombe huyo hali iliyopelekea ng’ombe huyo kuanza kupiga kelele
kwa kuomba msaada.
Ndipo wakazi wa eneo hilo walielekea eneo la
tukio na kumkuta kijana huyo akiendelea na kitendo hicho na kumshushia kipigo
cha mbwa mwizi mara baada ya kuvunja amri ya sita ya kuzini na ng’ombe huyo.
Aidha,kufuatia hali hiyo
Kijana Mwambusi aliomba msamaha kwa kitendo hicho lakini wananchi hao
hawakujali na mara akajikuta akimwagiwa maji ya baridi na kipigo kikiwa
kinaendelea na kusababishiwa maumivu sehemu mbalimbali ya mwili wake.
Hata hivyo wazazi wa
kijana huyo walijaribu kutoa kiasi cha shilingi 100,000 kwa wananchi hao ili
waweze kumwachia kijana wao kufuatia kipigo alichokuwa akipewa.
Kwa upande wake
mwenyekiti wa kijiji hicho Bwana Andongwisye Mwakalinga amethibitisha kutokea
kwa tukio hilo
na amewasihi wananchi hususani vijana kumwomba mungu muda wote ili kuondokana
na majaribu yasiyompendeza Mwenyezi Mungu.
0 comments:
Post a Comment