Amesema hayo mbele ya wajumbe
wa Mkutano Mkuu wa 8 wa CCM unaoendelea mjini Dodoma.
Kauli hiyo ya mwenyekiti wa ccm
ameitoa alipokuwa akifafanua kuhusu taarifa iliyosomwa na Naibu Waziri wa
Uchukuzi, Dkt. Charles Tizeba, mbele ya wajumbe hao kuwa serikali itajenga
kiwanja hicho.
Akitoa ufafanuzi huo, Rais
Kikwete amewaeleza wajumbe hao kwamba uwanja utakaojengwa utakuwa eneo la
Mugumu na sio kwenye Hifadhi ya Taifa ya Serengeti.
Amesema kuwa hatua hiyo ya
ujenzi wa kiwanja hicho cha ndege utawawezesha watalii uchaguzi wa ama kutua Mugumu au Uwanja wa
Kimataifa wa Kilimanjaro.
Amesema kwa watalii
watakaoshukia uwanja wa KIA na kutembelea hifadhi ya Tarangire, Manyara,
Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA) wataweza kuondoka kurejea makwao kwa
kutumia uwanja utakaojengwa Mugumu badala ya kurudi tena hadi KIA.
Hali kadhalika amesema, watalii
watakaoshuka kwenye uwanja utakaojengwa Mugumu hawatakuwa nahaja ya kurudi tena
Serengeti ili warejee makwao kwa kuwa wataendelea kutembelea vivutio vingine
kwenye katika Hifadhi za Manyara, Tarangire hadi Mlima wa Kilimanjaro na
kurejea makwao kwa kutumia uwanja wa KIA.
Akizungumzia kuhusu Uwanja wa
Ndege wa Kimataifa wa Songwe, dk kikwete amesema umekwishakamilika na uzinduzi
wake unatarajiwa kufanyika Desemba mwaka huu.
Amesema uwanja huo uko kusini
na yapo mashirika kadhaa ya ndege ya kimataifa ambayo yameomba ndege zao ziwe
zinatua kwenye uwanja huo wakati zikifanya safari zake za kwenda nchi za Kusini
mwa Afrika.
0 comments:
Post a Comment