Mwana
wa Rais wa zamani wa Malawi Bakili Muluzi amejiuzulu uwaziri serikalini.
Austine Atupele Muluzi
amejiuzulu uwaziri katika serikali ya Rais Joyce Banda wa nchi hiyo ikiwa ni
baada ya kutangaza nia yake ya kugombea katika uchaguzi ujao wa rais nchini
humo.
Atupele Muluzi alikuwa akihudumu kama Waziri wa Mipango ya Uchumi na
Maendeleo wa Malawi kama sehemu ya jitihada za bi. Banda za kugawa madaraka
kati ya vyama mbalimbali vya nchi hiyo. Mwana huyo wa Bakili Muluzi anakusudia
kugombea uraia kwa tiketi ya chama cha UDF katika uchaguzi ujao wa rais wa
mwaka 2014, chama ambacho kiliwahi kutawala Malawi chini ya uongozi wa baba
yake.
Atupele ametangaza hatua hiyo
baada ya wafuasi wa chama tawala kinachoongozwa na Banda cha People’s Party
(PP) kutoa matamshi mabaya kuhusu Bakili Muluzi na kuwataka watu kutomchagua
mtu ambaye hajui lugha ya Kiyao na kwamba hana hadhi ya kuwa rais wa nchi hiyo.
1 comments:
sindikumva zomwe mukuyakhula apazi! Mukuti bwanji?
Post a Comment