Serikali imekiri kuenea kwa tatizo la ubakaji
katika maeneo ya mjini na vijijini, na kuahidi kutafuta njia ya kukabiliana
nalo ikiwa pamoja na kutoa elimu kwa wananchi.
Akizungumza jijini Dar es Salaam kwa niaba ya
Waziri wa Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto, Sophia Simba, kwenye Tamasha la
Tanzania Alliance People’s Organization (TAPO), Naibu Katibu Mkuu wa wizara
hiyo, Anna Maembe, amesema kuwa ubakaji umekithiri hasa kwa watoto wadogo.
Amesema kuwa utandawazi ni miongoni mwa sababu
kubwa zinazochangia ubakaji na ulawiti, kutokana na kuongezeka kwa matumizi
mabaya ya mitandao ambapo inachangia ongezeko la vishawishi vya ubakaji.
Hata hivyo, aliwataka watoto kutoogopa vitisho
wanavyopewa kwa kuwa wanapaswa kutoa taarifa za matukio ya ubakaji
yanayowakumba.
Naye Mwenyekiti wa TAPO, Felista Nyakato amesema
kuwa, shirika hilo limeanzishwa kwa lengo la kukomesha na kutokomeza changamoto
za kijamii zinazowakabili watoto na vijana.
0 comments:
Post a Comment