SAKATA la watu wanaodaiwa ni wanandoa wasaliti kugandana, Temeke, Dar es
Salaam limechukua sura mpya baada ya kubainika kuwa, Mchungaji John
Mzule wa Kanisa la Gospel Revival Assemblies of God, Mbagala, Dar naye
alichangia kuenea kwa uvumi ule, hivyo polisi wanamfuatilia.
Mchungaji Mzule ameingia matatani baada ya kudaiwa kuwa, siku ya tukio
aliushawishi umma uamini kwamba kuna watu waligandana wakifanya zinaa
kwa vile alithibitisha kuwa, aliwaona wazinzi hao wakishushwa kutoka
kwenye gari aina ya Canter hospitalini Temeke.
Mchungaji huyo alikuwa akithibitisha hayo katika eneo la hospitali hiyo
pale alipohojiwa na mapaparazi hali iliyowafanya watu waliokuwa
wakimsikiliza kuamini hivyo na wao wakawapigia simu wenzao kutoka pande
mbalimbali za Jiji la Dar es Salaam ambao walifika kwa lengo la
kushuhudia.
Katika eneo la tukio, mwandishi wetu alimkuta Mchungaji Mzule akimlaumu
mtu aliyesababisha ‘wazinzi’ hao kugandana kwamba, alifanya kosa kubwa
sana na anastahili adhabu ya pekee atakapobainika.
TUNAMNUKUU: “Kitendo hiki ni cha kinyama sana na aliyesababisha hapaswi
kuvumiliwa kwa sababu ni udhalilishaji wa kijinsia.”
Uwazi lililokuwepo hospitalini hapo siku ya tukio, lilishuhudia wananchi
wakiwa wamefurika wakitaka kushuhudia watu hao waliogandana licha ya
kuambiwa na uongozi wa hospitali kwamba hakukuwa na tukio hilo.
Baadhi ya maafande wa Jeshi la Polisi waliozungumza na waandishi wetu
Novemba 9, 2012 walisema mtu aliyevumisha habari hiyo kama akijulikana
atachukuliwa hatua za kisheria kwa kosa la kuuadaa umma.
“Ni kwamba kama tutampata mchungaji huyo au mtu mwingine anayechangia
kueneza uvumi huu ni lazima tutamhoji atueleze kwa nini amezusha,”
alisema afisa mmoja wa cheo cha juu wa polisi ambaye hakutaka jina lake
liandikwe gazetini kwa kuwa siyo msemaji.
Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi wa Temeke, ACP Angelbert Kiondo alipopigiwa
simu siku ya Jumapili ili kusikia kauli yake juu ya tukio hilo, iliita
bila kupokelewa.
0 comments:
Post a Comment