Kutokana na kushamili kwa wimbi la
omba omba wengi katika jiji la Dar es Salaam chanzo chake kimeonekana ni
wanawake na watoto ndiyo wengi kama walivyonaswa na kamera ya Kajunason
Blog. Wanawake hao hukaa pembezoni mwa barabara na kuwatuma watoto wao
waende barabarani waombe na kuwaletea pesa. Pichani watoto wakisubiri
foleni za kwenye mataa ya Fire/Kariakoo jiji Dar es Salaam.
Mtoakiomba mara baada ya daladala kusimama.
Watoto wengine hukimbilia magari madogo.
Watoto wakikomaa kuomba.
Wengine nao wakikimbilia gari ili waombe.
Akina mama waliwa wamekaa pembeni ya barabara wakisubiri watoto wao wawaletee hela walizoomba.
Ni aibu ila hakuna jinsi...
Mama akina akimtoa mwanae barabarani mara baada ya kuona kamera imemuulika.
Akina mama wengine waliamua kuondoka eneo hilo mara baada ya kuona wanapigwa picha.
Watoto
wakiwa wamekaa pembezoni mwa barabara wakisubiri magari, hali ambayo ni
hatari sana. Serikali haina budi kuchukua hatua kazi kwa watu hawa ili
kuweza kukomesha omba omba ambao kwa sasa wametanda pembezoni mwa
barabara za jiji la Dar.
0 comments:
Post a Comment