Ndugu zangu,
Kwa miaka mitatu au minne sasa nimekuwa nikifuatilia taarifa mbalimbali - kitaifa na kimataifa, kwamba mwaka huu 2012 kuna tukio kubwa litakalotokea.
Kupitia kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii tumeelezwa kuhusu 'Ujio wa Mpinga Kristo', na hapa ndipo tumeweza kushuhudia mwaka huu kwamba kumbe ule mtandao wa siri wa Freemason na Illuminati umejitokeza hadharani ambapo baadhi ya Watanzania wamefikia hatua ya kusema wao ni mawakala wa kusajili wanaotaka kujiunga na imani hiyo, ambayo kwa miaka mingi imekuwa ikitambulika kama ni 'Dini ya Mashetani'!
Yamesemwa mambo mengi kuhusiana na watu mbalimbali wenye mafanikio nchini kwamba ni wafuasi wa Freemason, hivyo utajiri wao ni 'wa kishetani'.
Lakini kumbe hilo siyo tukio lililokuwa likisemwa, hasa baada ya kuibuka kwa taarifa nyingine kwamba, mwaka huu 'Ndio Mwisho wa Dunia' kwani sayari yetu itagongana na 'sayari' nyingine. Hii ni kwa mujibu wa kalenda mbalimbali za kale kama za Wamaya wa huko Marekani ya Kusini na hata Kalenda ya Kale ya Babeli.
Wapo waliosema siku hiyo ingekuwa Julai 21, 2012, wengine wakasema ingekuwa Novemba 21, 2012, lakini wanaorejea Kalenda ya Wamaya wanasema itakuwa Desemba 21, 2012, yaani siku 13 kutoka leo.
Wanasayansi wanasema 'sayari' hiyo inaitwa Nibiru, au Sayari Nyekundu ama Sayari X, ambayo kimsingi ni Kimondo ambao wanabainisha kwamba inaweza kugongana ama kunusurika kidogo kugongana na Dunia.
Lakini waamini wa 'Siku za Mwisho' wanaamini kwamba, Nibiru ndiyo Nyota inayotajwa kwenye Kitabu cha Ufunuo wa Yohana, Sura ya 8:10-12 ambao unaeleza: "10 Malaika wa tatu akapiga baragumu, nyota kubwa ikaanguka kutoka mbinguni, iliyokuwa ikiwaka kama taa, ikaanguka juu ya theluthi ya mito, na juu ya chemchemi za maji.
11 Na jina lake ile nyota yaitwa Pakanga; theluthi ya maji ikawa pakanga, na wanadamu wengi wakafa kwa maji hayo, kwa kuwa yalitiwa uchungu. 12 Malaika wa nne akapiga baragumu, theluthi ya jua ikapigwa, na theluthi ya mwezi, na theluthi ya nyota, ili kwamba ile theluthi itiwe giza, mchana usiangaze theluthi yake, wala usiku vivyo hivyo."
11 Na jina lake ile nyota yaitwa Pakanga; theluthi ya maji ikawa pakanga, na wanadamu wengi wakafa kwa maji hayo, kwa kuwa yalitiwa uchungu. 12 Malaika wa nne akapiga baragumu, theluthi ya jua ikapigwa, na theluthi ya mwezi, na theluthi ya nyota, ili kwamba ile theluthi itiwe giza, mchana usiangaze theluthi yake, wala usiku vivyo hivyo."
Kwa maana nyingine, inaelezwa kwamba huo ni mwanzo wa Mwisho wa Dunia.
Pamoja na taarifa hizo, ambazo kimsingi zinaweza kuzusha wahaka kwa Watanzania wenzangu na mimi, kamwe sijasikia kauli kutoka kwa wanasayansi wetu wakilizungumzia tukio hili, ambalo linaweza kuzusha hali tete kama halikubainishwa na watalaamu hao.
Sijui, hivi kuna yeyote mwenye taarifa sahihi juu ya jambo hili au ni udaku wangu na upekenyuzi ndio unaonifanya nifuatilie kwa karibu? Mwisho wa Dunia sijui, kwa sababu ndivyo hata vitabu Vitakatifu vinavyotueleza, lakini ikiwa tukio hili ni la kisayansi na litatokea kweli, naamini jamii ina kila sababu ya kupewa taarifa na wataalamu wetu, waliosomeshwa kwa kodi zetu na za baba zetu.
0 comments:
Post a Comment