Pages

Home » » JUMAPILI YA LEO, JE UNAFIKIRI NINI KUHUSU MAMLAKA NA UKUU WA MANGU NA MAIKA WAKE......Kuasi Kwa Shetani Ni Makusudi Ya Mungu!??

JUMAPILI YA LEO, JE UNAFIKIRI NINI KUHUSU MAMLAKA NA UKUU WA MANGU NA MAIKA WAKE......Kuasi Kwa Shetani Ni Makusudi Ya Mungu!??

PICHA HAINA UHUSIANO KAMILI LAKINI HUO NI MFANO WA YESU NA SHETANI WAKIPIMANA NGUVU, HII ILIJITOKEZA HASA WAKATI WA UKOMBOZI WA MWANADAMU
 

Wajumbe wenzangu,
Kadiri tunavyoambiwa kwamba hizi ni siku za mwisho ndivyo ambavyo watu wanaendelea kutenda dhambi kama kwamba mafundisho yote ya Vitabu Vitakatifu yamekuwa bure tu. Lakini wapo baadhi ya watu ambao wameamua kwa nia njema kabisa kuzama kwenye Vitabu hivyo na kuyatafakari Maneno ya Mungu ili kujua Kweli yake.
Nimekutana na maswali mengi, lakini kubwa zaidi ambalo limenifanya nililetea barazani ni hili: Tunatambua Mungu aliuumba ulimwengu kwa nia njema, akamuumba Adamu kwa mfano wake ili amtumikie, kumwabudu na kumcha Yeye pekee Yehova.
Lakini katika Maandiko hayo hayo, hasa baada ya Adamu 'kuletewa' msaidizi wake Hawa, ghafla tunaona kwamba Adamu na mkewe wanatenda dhambi kubwa na kulaaniwa kwa hukumu ya KIFO.
Maandiko mengine yanasema kwamba, Shetani, ambaye ndiye aliyemhadaa Hawa na kumfanya yeye na Adamu watende dhambi kubwa, alikuwa Malaika wa Mungu kwa jina la Lucifer, akikaa pembeni kabisa ya Mungu, lakini akaasi na kufukuziwa Kuzimu.
Kwa vile masuala haya ni mazito na yanahitaji Imani, ingekuwa vyema ikiwa wanazuoni wakatueleza bayana, hivi kuasi kwa Shetani hakukuwa kusudio la Mungu? Hivi kuzimu haikuwekwa makusudi tu kabla ya kuumbwa kwa ulimwengu ili kwamba kuwepo na namna ambayo mwanadamu atatambua kwamba yupo Mungu? Ni kweli kwamba wote walitakiwa kuiona na kuishi ndani ya Yerusalemu Mpya? Kama ndivyo, ilikuwaje basi Mungu akauweka mtihani wa kuasi kwa Shetani na kuwaacha wanadamu wakitangatanga?
Haya ni mawazo yangu tu, mnaweza kunielewesha vizuri, maana naamini humu ndani wanapita pia wanazuoni. Msinikasirikie, kwani aulizae ataka kujua, na kwa siku hizi za mwisho, ni vizuri tukajifunza na kumrejea Mungu.

Mjumbe mwenzenu,
Mbega Mnyama.
Jika Anda menyukai Artikel di blog ini, Silahkan klik disini untuk berlangganan gratis via email, dengan begitu Anda akan mendapat kiriman artikel setiap ada artikel yang terbit di Creating Website

0 comments:

Post a Comment

 
Support : Greyson Salufu | Chimbuko Letu Inc | Chimbuko Letu Inc
Copyright © 2011. Mbwile Media - All Rights Reserved
Template Modify by Chimbuko Letu Inc
Proudly powered by Blogger