Pages

Home » » KANDORO AVUNJA UKIMYA KWA VIONGOZI WA DINI DHIDI YA UCHOCHEZI WA KIDINI

KANDORO AVUNJA UKIMYA KWA VIONGOZI WA DINI DHIDI YA UCHOCHEZI WA KIDINI



Mkuu wa mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro amewataka waislamu kushirikiana na kujenga umoja miongoni mwao badala ya kutengeneza majungu ambayo yanaathiri maendeleo yao.

Bw. Kandoro alizungumza hayo wakati wa uzinduzi wa Kituo cha Mfuko wa Maendeleo cha mkoa wa Mbeya MRIDEF kilichopo Sokomatola jijini Mbeya jana asubuhi.

Alisema kuwa waislamu wamekuwa hawana kawaida ya kujituma katika maendeleo hali ambayo inachangia kwa asilimia kubwa kurudisha maendeleo hivyo aliwataka kujikita katika kazi katika maeneo yao ili kuepuka malalamiko ya kutengwa katika shughuli za maendeleo.

'' Jishughulisheni kwenye kazi za maendeleo na ujasiriamali, tusome elimu zote za dini na dunia, tuwasomeshe watoto wetu wapate elimu zote za dunia na akhera''alisisitiza Bw. Kandoro.

Alisema kila mzazi aangalie fursa zinazomzunguka ili ajijengee uchumi katika kaya yake na kumudu huduma za msingi na kujiongezea kipato halali.

Kwa upande wake Katibu wa mfuko wa Maendeleo ya Waislamu Mkoa wa Mbeya Shekhe Abbas Mshauri alisema kuwa madhumuni ya Taasisi hiyo ni kusaidia kuleta maendeleo ya kijamii na kidini na kuongeza elimu na uchumi wa kila mmoja kulingana na maadili ya Uislamu.

Alisema kuwa taasisi imedhamiria kuweka vitega uchumi na mahusiano na ushirikiano na asasi zingine za kidini Kitaifa na Kimataifa.

Kwa hisani ya Rashidi Mkwinda
Jika Anda menyukai Artikel di blog ini, Silahkan klik disini untuk berlangganan gratis via email, dengan begitu Anda akan mendapat kiriman artikel setiap ada artikel yang terbit di Creating Website

0 comments:

Post a Comment

 
Support : Greyson Salufu | Chimbuko Letu Inc | Chimbuko Letu Inc
Copyright © 2011. Mbwile Media - All Rights Reserved
Template Modify by Chimbuko Letu Inc
Proudly powered by Blogger