GWARIDE LA MAJARIBIO LA MAADHIMISHO YA MIAKA 51 YA UHURU WA TANZANIA
Kikosi
cha Gwaride cha Jeshi la wananchi la Tanzania (JWTZ) Kikipita mbele ya
maofisa wa Vyombo vya ulinzi na Usalama wakati wa gwaride la majaribio
la kuadhimisha miaka 51 ya Uhuru wa Tanzania katika uwanja wa Uhuru leo
asubuhi ambapo keshokutwa Desema 9 mwaka huu maadhimisho hayo
yatafanyika katika uwanja huo Mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Rais wa
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Dkt. Jakaya Mrisho
Kikwete.
Kikosi cha jeshi la Magereza kikipita mbele ya maofisa hao
Kikosi cha Bendera kutoka Jeshi la Wananchi la Tanzania JWTZ kikipita.
Kikosi cha Wanamaji kikitembea kwa Mwendo wa Polepole.
………………………………………………………..
Na. Aron Msigwa – MAELEZO.
Dar es salaam
Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam
Saidi Meck Sadiki amewaomba wakazi wa jiji la Dar es salaam kujitokeza
kwa wingi kuhudhuria sherehe za maadhimisho ya miaka 51 ya Uhuru wa
Tanganyika zitakazofanyika katika Uwanja wa Uhuru jiji Dar es salaam.
Akitoa ufafanuzi wa kukamilika
kwa maandalizi ya sherehe hizo leo jijini Dar es salaam Bw. Saidi Meck
Sadiki amesema kuwa maadhimisho ya mwaka huu yatahudhuriwa na
viongozi mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi na mwaka huu mkoa wa
Dar es salaam umepewa heshima ya kuandaa sherehe za kutimiza miaka 51 ya
uhuru.
Amesema katika kipindi cha
miaka 51 ya uhuru Tanzania imepata mafanikio makubwa katika nyanja
mbalimbali za uchumi, ulinzi na usalama pamoja na uhusiano wa
kimataifa.
Amefafanua kuwa
mgeni rasmi katika maadhimisho hayo atakuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania Dkt.Jakaya Kikwete na kuongeza kuwa yataongozwa na kauli
mbiu isemayo Uwajibikaji, Uadilifu na Uzalendo ni nguzo ya Maendeleo ya
Taifa letu.
Aidha amefafanua kuwa sherehe za
mwaka huu zitahudhuriwa na ugeni wa marais kutoka Jumuiya ya Nchi za
Kusini mwa Afrika (SADC) na kupambwa na gwaride maalum lililoandaliwa na
vikosi vya ulinzi na usalama vya Tanzania , halaiki maalum, vikundi
mbalimbali vya burudani vya ngoma za asili vya hapa Tanzania hususani
kutoka maeneo ya Ukerewe, Dodoma na Zanzibar.
Vikundi vingine vitakavyopamba sherehe hizo ni kundi la Taifa la sanaa kutoka nchini Rwanda (Rwanda National Ballet).
0 comments:
Post a Comment