Matukio
ya ubakaji watoto wadogo yameendelea kujirudia mkoani hapa baada ya mtoto wa
(jina tunalihifadhi) mwenye umri wa miaka 2 na miez 6 mkazi wa Ilboru kubakwa hadi kulazwa kwenye hospitali ya mkoa ya
Mount Meru jijini Arusha.
Tukio
hilo la kutisha limetokea jana majira ya asubuhi kwenye mtaa huo wa Ilboru kwa
kijana wa miaka 20 nae ni mkazi wa mtaa
huo kufanya kitende hicho cha kinyama baada ya mama wa motto huyo kutoka na
kumuacha mtoto huyo akicheza na wenzake na ndipo mtuhumiwa huyo kujifanyia
anavyotaka kwa mtoto huo.
Akizungumza
na waandishi wa habari kwenye hospitali ya mkoa mama wa mtoto huyo aitwae Mariam
Miller mwenye umri wa miaka 30 alisema kuwa yeye alipotoka kidogo kumsindikiza
jirani yake aliporudi alimkuta mtuhumiwa akiwa anavaa suruali baada ya kumaliza
kitendo hicho huku motto wake akilia kwa nguvu hali iliyomshitua na ndipo
alipoanza kumuuliza mtuhumiwa lakinmi alianza kukimbia bila ya kutoa
majibu.
Alisema
kuwa alipo mkagua alimkuta mwanae ana mabaki ya manii kwenye sehemu zake za siri
na ndipo alipowaeleza nduguze
waliomshauri kumpeleka hospitali kwa matibabu na hivyo walimpeleka hospitalini
hapo kwa matibabu zaidi lakini kabla ya kupewa huduma wauguzi hospitalini hapo
walimtaka kupeleka PF3 ya polisi na ndipo alitoa taarifa polisi.
Wakati
waandishi wapo wakiendelea kumuhoji mama huyo walipata taarifa za mtoto mwengine
wa kike mwenye umri wa miaka 10 (jina tunalihifadhi) aliyebakwa na kijana wa
miaka 30 wote wakazi wa mtaa wa Pangani kata ya kati jijini hapa na kesi yake
ipo polisi kwa uchunguzi.
Akielezea
mbele ya waandishi wa habari bibi wa mtoto huyo Zahra Mohamed alisema kuwa yeye
anajishughulisha na biashara ya kuuza vitafunwa kwenye stand kuu ya mabasi
jijini hapa alipotoka kweda kwenye shughuli zake kuna kijana wa nyumba ya jirani
huwa anakuja nyumbani hapo mara kwa mara kama nyumbani lakini hakugundua kama
kuna mchezo mchafu unaendelea nyuma wakati akitoka lakini za nmwizi arubaini
juzi majira ya jioni alirudi nyumbani ghafla ndipo alimkuta kijana huyo uani
kwao na binti alipomwita alichelewa kuja na alipokuja alikuwa na wasiwasi mwingi
ndipo mama yake mkubwa alianza kumchapa ili amweleze kwanini analia na kuwa na
wasiwasi ndipo alipomba asichapwe ataeleza ukweli
Zamzam
alisema kuwa hiyo si mara ya kwanza bali kila mara kijana huyo aliyefahamika kwa
jina Moja la Yasin alikuwa akimuingilia na kumpa shilingi mia mbili kama ujira
wa kufanya nae kitendo hicho huku akimtisha akisema atampeleka
polisi.
Wakizungumza
kwa nyakati tofauti wazazi na walezi hao walisema kuwa wanaiomba serekali mkoani
hapa kuyacvhukulia kwa uzito matukio hayo ya ukatili wa kuwabaka watoto wadogo
kwani kwa siku za hivi karibuni matukio hayo yamekithiri kwenywe mitaa mbali
mbali ya jiji hili
Kamanda
wa Polisi Liberatu Sabas alisema kuwa jeshi la polisi mkoani hapa linaendelea na
uchunguzi wa matukio hayo na kuwa watuhumiwa wote wakikamatwa watafikishwa kwenye vyombo vya sheria ili
sheria ichukuwe mkondo wake na kuwataka wakinamama kuwa karibu na watoto wao ili
kuweza kubaini au kukabiliana na vitendo hivyo.
Imeandikwa
na Mahmoud Ahmad, Arusha-Tanzania.
0 comments:
Post a Comment