Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Jakaya Mrisho Kikwete anatarajiwa
kufungua Mkutano wa Kimataifa wa wadau wa chanjo duniani (GAVI) unaoanza leo
.
Mkutano
huo unatarajiwa kuwa washiriki 600 kutoka nchi mbalimbali duniani wakiwemo wake
wa Marais , Mawaziri wa Afya, fedha na watu mashuhuri kutoka nchi
73.
Kwa
mujibu wa taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa leo mjini Dar es salaam na
Kaimu Katibu Mkuu Regina Kikuli inasema kuwa lengo la mkutano huo ni pamoja na
kujadili mafanikio na changamoto zinakabili huduma ya utoaji wa chanjo
duniani.
Taarifa
hiyo inaongeza kuwa hii ni mara ya kwanza mkutano wa aina hiyo kufanyika Afrika
mashariki na kuongeza kuwa sababu zilizopelekea mkutano kufanyika Tanzania ni
pamoja na mafanikio makubwa katika utoaji wa huduma za chanjo za watoto na mama
wajawazito.
Hivyo
basi washiriki watapata fursa ya kutembelea vituo vinavyotoa huduma za chanjo
nchini ili kujionea mafanikio na changamoto zilizopo pamoja na
kujifunza.
Vilevile
washiriki watapata fursa ya kujadili masuala ya chanjo ikiwemo uingizwaji wa
chanjo mpya na masuala ya afya ya mama na mtoto.
Pia
kutakuwepo na uzinduzi wa chanjo mbili mpya za magonjwa ya kuhara, homa ya uti
wa mgongio kwa watoto chini ya mwaka mmoja ambazo zinatolewa nchini kwa hisani
GAVI
0 comments:
Post a Comment