Gari moshi likikaribia kufika stesheni ya Mwanza
|
Jengo la Shirika la Reli Mwanza |
|
Tangazo likionyesha kuanza kwa safari za gari moshi |
|
Abiria wakishuka baada ya gari moshi kufika steshen ya mwanza |
|
Raia wa kigeni nao walikuwa miongoni mwa abiria waliowasili na gari moshi |
|
Waandishi wa habari wakizungumza na naibu waziri wa uchukuzi Dk. Charles Tizeba |
|
Moja ya mabehewa ya Gari Moshi |
|
Wananchi waliofika kushuhudia kufika kwa gari moshi kwenya stesheni ya mwanza |
|
Moja ya behewa la gari moshi likiwa katika hali mbaya |
|
Naibu waziri wa uchukuzi Dk. Charles Tizebaakitoka kuzindua safari za gari moshi |
|
Salamu kwa Dk Mwakyembe |
Shikamoo
Dk Mwakyembe, habari ya Jumapili najua utakuwa umepumzika leo jumapili
baada ya majukumu ya wiki iliyopita , mimi rafiki yako Mkami Jr baada
ya kutoka kukusaidia kazi ya kukagua Reli ya Moshi, Nimeamua nisafiri
mpaka kanda ya ziwa nikusaidie tena kazi ya kukagua.
Dk
Mwakyembe najua utashangaa kwanini nimejipa kazi hii bila kupewa kibali
cha ofisi yako (Wizara ya uchukuzi), binafsi mimi nimejiajiri kufanya
kazi zote za umma hivyo nadhani hata kazi hii ya kuja mwanza kukagua
reli ni moja ya majukumu yangu kama mfanyakazi wa umma nisiye na ofisi
wala mshahara au posho ya safari Dk mwakyembe usije shangaa siku
nyingine nikafika hadi bandarini nikusaidie kupunguza msongamano wa
makontena kwa kazi hizi nazofanya sihitaji kusifiwa, sihitaji posho ila
nimeipenda tu kazi hii.
Dk
Mwakyembe kama ambavyo niliyoona hali ya reli kule Moshi ambapo
nilikuta Reli na majengo mabovu na behewa moja tu na sikuona dalili
zozote za reli ile kufanya kazi na wala sikuona matumaini kama kuna siku itafanya kazi.
Leo
hii Dk Mwakyembe umeniwahi huku Mwanza sina budi kukupongeza wewe na
timu yako kwa kazi nzuri kazi nzuri mnayofanya, leo nimeona Gari moshi
likifika stesheni ya Mwanza na nimeomuona Naibu Waziri wako Dk Dk.
Charles Tizeba akizungumzia ujio wa safari za Gari moshi huku akisema
maneno yenye kutia matumaini ikiwemo kuboresha usafiri huo kadri uwezo
unapopatikana ni maneno ya faraja naamini amezungumza kwa niaba ya ofisi
yako hivyo nawe unahusika kutekeleza aliyoyasema msaidizi wako,
Pamoja
na sifa ambazo wananchi wanakumwagia ila Rafiki yangu Dk Mwakyembe kazi
ngumu ipo mbele yako ndio maana nikaona nikusaidie baadhi ya mambo ,
Jambo kubwa ambalo wananchi wamekuwa wakizungumzia usafiri huu ambao
kwao ni ukombozi ni jambo la kuhujumiwa , mfano leo nimesikia kuwa wenye
mabasi hutumika kuhujumu miundombinu ya reli na kufanya gari moshi
kusimama kufanya kazi mara kwa mara, Sina ushahidi kuhusiana na jambo
hili ila waswahili walisema lisemwalo lipo kama halipo laja..
Nikutakie
kazi njema Dk harrison Mwakyembe na msaidizi wako Dk. Charles Tizeba
na timu yako ya wizara ya uchukuzi na timu nzima ya Shirika la reli kwa
kazi nzuri mnayoifanya ila inabidi mjipange kukabiliana na changamoto
ikiwamo hujuma katika miundombinu na kuboresha magari moshi hapa nikiwa
na maana kukarabati injini za gari moshi na kukarabati mabehewa yawe ya
kisasa zaidi.
Asante
sana Dk Mwakyembe nikutakie mapumziko mema ya weekend na fikisha
salamu zangu kwa familia yako bila kumsahau dereva wako na kesho ukiwa
ofisini fikisha salamu zangu kwa Katibu Muhtasi wako hawa ni watu muhimu
pia kwenye kazi yako
0 comments:
Post a Comment