RAIS Jakaya Kikwete amewataka
Watanzania kujivunia na kuyaenzi mafanikio ya kisiasa, kiuchumi na
kijamii, yaliyopatikana tangu nchi ilipojipatia uhuru wake mwaka 1961.
Akizungumza kwenye maadhimisho
hayo ya mika 51 ya uhuru wa Tanzania Bara, uliofanyika kwenye uwanja wa
Uhuru jijini Dar es Salam leo, Rais Kikwete alisema yamekuwa tofauti na
ya awali, safari hii yakihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa kuu kutoka
nchi 14 za Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC).
Alisema mafanikio hayo yametokana na uvumilivu wa kisiasa ujengeka miongoni mwa Watanzania.
Kikwete alisema katika miaka 51
ya uhuru wa nchi hiyo, imekuwa katika utulivu na amani ambapo utulivu
huo umekuwa chachu ya maendeleo katika jamii ya Watanzania.
Aidha, viongozi waliohudhuria
maadhimisho hayo, Rais Kikwete amewataja kuwa ni pamoja Rais wa Jamhuri
ya Congo (DRC), Joseph Kabange Kabila, Emilio Armando Guebuza,
(Msumbiji), na Hifikepunye Pohamba (Namibia), mbaye alishuhudia
Tanzania Bara ikipata uhuru mwaka 1961 na Makamu wa Rais wa Zambia Guy
Scott.
Wengine ni Makamu wa Rais wa
Angola Manuel Domingos, Waziri Mkuu wa Rwanda, Pierre Au Moyen, Waziri
Mukuu wa Swazland, Sibusiso Dlamini, Simba rashe na wengine.
Katika sherehe za maadhimisho
hayo kulikuwa na burudani mbalimbali ikiwemo gweride la vikosi vya
Majeshi, Halaiki ya watoto na ngoma za asili pamoja na kikundi cha Taifa
cha ngoma za asili kutoka Rwanda.
Naye Katibu wa Itikadi na Uenezi
wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Nape Nnauye amekiri kuwa miaka 51 ya
uhuru bado nchi inakabiliwa na changemoto mbalimbali ingawa yapo
mafanikio katika huduma nyingi za kijamii.
Pia amevitaka vyama mbalimbali
vya siasa kutobeza kila mafanikio yaliyopatikana katika nchi hiyo bali
vijaribu kuja na njia mbadala zitakazolisaidia taifa katika kuwakwamua
wananchi katika changamoto hizo kwani maendeleo ni ya Wanzania wote .
Alisema serikali hii imefanya mambo makubwa katika upande wa elimu pamoja na miundombinu ya barabara hivyo ni vyema ikapongezwa.
Kwa Upande wake Mwenyekiti wa
Chama cha Mageuzi (NCCR Mageuzi), James Mbatia pamoja na kusherehekea
miaka 51 bado inchi inakabiliwa na changamoto ya umasikini uliyopitiliza
na kuwa ufukara.
Alisema asilimia 30 ya
watanzania bado wanakula mlo mmoja kutokana na kukabiliwa na ufukara
hivyo kuna ulazima kwa serikali kuwekeza zaidi kwenye elimu kama chachu
ya kuwakwamua wananchi hao katika kuondokana na ufukara huo.
Katika hatua nyingine ya maadhimisho hayo ya miaka 51 ya uhuru, Rais Kikwete ametoa msamaha kwa wafungwa 3814.
Akizungungumza kwa niaba ya
Rais, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk. Emmanuel Nchimbi, alisema
Rais ametumia madaraka aliyopewa chini ya Ibara ya 45(1), ya Katiba ya
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Aliwataja wafungwa walionufaika
na msamaha huo kuwa ni pamoja na wale wanotumikia kifungo kisichozidi
miaka mitano ambao hadi Desemba 9 mwaka huu wamekwishatumikia robo ya
vifungo vyao.
Wengine ni wagonjwa wa Ukimwi,
kifua kikuu, (TB),saratan na kundi la wafungwa wa wanawake walioingia
gerezani wakiwa na ujauzito na wale walioingia wakiwa na watoto
wanaonyonya na wasiyonyonya.
Dk Nchimbi aliongeza kuwa kundi jingine ni la wafungwa wenye ulemavu wa mwili na akili.
Aidha msamaha huo wa Raisi
hautawahusu wafungwa waliohukumiwa kunyingwa, wanaotumikia kifungo cha
maisha, wa makosa ya kujihusisha na biashara ya dawa za kulevya kama
vile cocaine, heroine, bangi na mengine.
Wengine ni wafungwa wanaotumikia
kifungo kutokana na makosa ya kupokea au kutoa rushwa na wa makosa ya
kunajisi, ubakaji, kulawiti, makosa ya unyang’nyi wa kutumia silaha na
wale waliopatikana na hatia ya kuwapa mimba wanafunzi wa shule za mzingi
na sekondari ambao walitenda kosa hilo wakiwa na umri wa miaka 18.
0 comments:
Post a Comment