WILAYA YA CHUNYA – WATU 13 WAKAMATWA
NA KUFIKISHWA MAHAKAMANI
KUTOKANA NA VURUGU ZILIZOPELEKEA UHARIBUFUWA
MALI [YAKIWEMO MASANDUKU YA KURA] NA UPORAJI.
MNAMO TAREHE 08/12/0212 MAJIRA YA SAA
17:15HRS HUKO KATIKA KIJIJI CHA SAZA –KATIKA OFISI YA AFISA MTENDAJI KATA YA
SAZA - MKWAJUNI WILAYA YA CHUNYA MKOA WA MBEYA. BAADHI YA WANANCHI WA KIJIJI
HICHO WALIAMUA KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI KWA KUFANYA FUJO NA KUSABABISHA UHARIBIFU
WA MALI ZIKIWEMO GARI NO SM 3830AINA YA TOYOTA L/CRUISER MALI YA HALMASHAURI YA
WILAYA YA CHUNYA,IKIWA NI PAMOJA NA KUVUNJWA KIOO CHA MBELE, OFISI YA AFISA
MTENDAJI WA KATA YA SAZA KUVUNJWA MLANGO, OFISI YA AFISA MTENDAJI KIJIJI CHA
SAZA KUVUNJWA MLANGO NA MASANDUKU 24 YA KUPIGIA KURA KUHARIBIWA. THAMANI HALISI
YA UHARIBIFU HUO BADO HAIJAFAHAMIKA. CHANZO CHA UHARIBIFU HUO NI KUSHINIKIZA
KUZUIWAKUFANYIKA KWA UCHAGUZI MDOGO WA NAFASI YA MWENYEKITI WA KIJIJI NA VITONGOJI.
KUFUATIA TUKIO HILO WATUHUMIWA KUMI NA TATU WAMEKAMATWA AMBAO NI PAMOJA NA {1} BENADETHA D/O ZAKARIA MIAKA 38 DIWANI VITI MAALUM CHADEMA KATA
YA SAZA {2} JOHN MPONZAYO ,MIAKA 52,
MUHA MKULIMA {3} SELEMANI TANGANYIKA,MIAKA
24,MNYIHA {4} AMBOKILE FRANCIS,MIAKA
23,KYUSA,MKULIMA {5} AMOSS/O JOSEPH,MIAKA
24,MNYAMWEZI,MKULIMA{6} ABDUL
MWANDEULE,MIAKA 20,KYUSA,MKULIMA{7}
CHRISTOPHER MWANJAYO,MIAKA 37,KYUSA,MKULIMA {8} BRAISON S/O MWASIMBA,MIAKA
34,KATIBU WA CHADEMA KATA YA SAZA {9}
BARAKA S/O SAULI,MIAKA 19,KYUSA,MKULIMA {10}
MUSSA S/O MNYONGA,MIAKA 32,MBUNGU {11}
ESSA S/O PIUSI,MIAKA 18,MBUNGU,MKULIMA {12} MARCO S/O GIBSON,MIAKA
25,MNYIHA,MKULIMA NA {13}PARADISO
S/O EMANUEL,MIAKA 26,MSAFWA,MKULIMA MKAZI WA NJELENJE WILAYA YA MBEYA VIJIJINI.
KUFUATIA
HALI HIYO YA UVUNJIFU WA AMANI UCHAGUZI HUO UMEAHIRISHWA NA BADALA YAKE UTAFANYIKA
LEOJUMATATU TAREHE 10/12/2012.TARATIBU ZA KISHERIA ZIMEFANYIKA NA WATUHUMIWA
WOTE 12 WAMEFIKISHWA KATIKA MAHAKAMA YA WILAYA YA CHUNYA LEO TAREHE 10.12.2012
NA KUSOMEWA MASHTAKA YA KUFANYA FUJO NA KUHARIBU MALI KIOO CHA GARI SM 3830
AINA YA TOYOTA L/CRUISER MALI YA HALMASHAURI YA WILAYA YA CHUNYA, KUHARIBU
MILANGO YA OFISI YA MTENDAJI KATA NA KIJIJI CHA SAZA, KUHARIBU MASANDUKU 24 YA
KUPIGIA KURA.AIDHA WATUHUMIWA NAMBA 5, 8
NA13WAMESOMEWA MASHTAKA YA ZIADAYA
UNYANG’ANYI WA PESA TSHS 2,150, 000/= AMBAZO ZILIKUWA NI SEHEMU YA GHARAMA ZA
UCHAGUZI NA SIMU YA KIGANJANI PAMOJA NA
SAA YA MKONONI MALI YA WESTON S/O NJENJE, MIAKA 52, MNYIHA, AFISA UCHAGUZI.
KAMANDA
WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI ANATOA WITO
KWA JAMII KUACHA TABIA YA KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI NA BADALA YAKE WAHESHIMU
NA KUTII SHERIA BILA KUSHURUTISHWA. AIDHA ANATOA RAI KWA MTU/WATU WENYE KERO
/MALALAMIKO KUTAFUTA NJIA HALALI ZA
KUFIKISHA KERO/MALALAMIKO YAO KWA NJIA YA MAZUNGUMZOAMA KWA KUFUATA SHERIA BADALA YA KUTUMIA VURUGU/FUJO NA KUSABABISHA
HASARA NA UHARIBIFU WA MALI ZA SERIKALI KWANI HALI HIYO INARUDISHA NYUMA
MAENDELEO YAO. PIA AMEENDELEA KUSISITIZA KUWA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KAMWE
HALITAVUMILIA MATUKIO YA NAMNA HII KUENDELEA KUJITOKEZA .AMEENDELEA KUWAHIMIZA WANANCHI WALIOWEMA AMBAO NI WENGI KUUNGA MKONO JITIHADA
HIZO KWA KUTOWAUNGA MKONO WAVUNJAJI SHERIA.
0 comments:
Post a Comment