Mbolea iliyobaki katika kijiji cha Mdandu aina ya minjingu mazao ambayo baadhi ya wananchi hawana imani nayo kutokana na historia ya kipindi cha nyuma.
Hizo ni
mbolea zilizobaki baada ya wakulima kugoma kuzichukua huko mdandu
kutokana na serikali kuwataka wakulima kuchukua seti nzima wakati
imecheleweshwa.
Na.Mwandishi wetu, Njombe.
Wakazi wa tarafa ya Mdandu wilayani Wanging’ombe wamegoma
kuchukua mbolea za ruzuku zinazotolewa na serikali kutokana na kufika wakati
wakiwa wamekwisha panda mazao.
Katibu tarafa wa kata ya Mdandu Benson Wandelage akizungumza
na kituo hiki amesema wakulima wengi tarafani humo wameamua kuacha kuchukua
mbolea hizo kutokana na kuja huku wakiwa wamepanda, na kwamba kwa sasa
wanahitaji mbolea za kukuzia za urea.
Bwana Wandelage
amesema tarafa ya Mdandu wananchi
wachache tu wamejitokeza kuchukua mbolea hizo lakini wengine hawataki kabisa
kuchukua kwa madai kwamba wanahitaji urea tu, lakini sasa kwa utaratibu wa
serikali mtu hawezi kuchukua mbolea nyingine wala mbegu bila kuchukua mbolea za
Minjingu mazao,
Wakazi wa mkoa wa Njombe licha ya mbolea za ruzuku kuchelewa,
lakini wamekuwa wakisuasua kutumia mbolea ya Minjigu Mazao kutokana na kutokuwa
na imani nayo baada ya kuitumia mara ya kwanza ikiwa Mijinjingu kuwasababishia
kupata mazao duni.
Ameeleza kuwa kwa sasa mkuu wa wilaya hiyo Esterina Kilasi
amewaagiza wataalamu wa ugani kuwa na shamba la mfano kwa ajili yakutolea elimu
kwa wakulima katika maeneo yao
ikiwemo kufanya majaribio ya vitendo kwa kutumia mbolea hizo za minjingu mazao.
Hata hivyo wataalam wa kilimo wamekuwa wakijaribu kutoa
elimu kwa wakulima juu ya mbolea hiyo, juhudi ambazo bado hazijazaa matunda ya
kutosha katika kubadilisha fikra za wakulima za kujenga imani na mbolea hiyo.
Mbolea ya minjingu mazao awali ilidaiwa kutokuwa na madini
ya nitrogen, lakini licha ya kuboreshwa kwa kuwekewa madini hayo wananchi
wameendelea na msimamo wa kutokuwa na imani nayo, hali ambayo imepelekea ugumu
katika ugawaji wa mbolea za ruzuku mkoani hapa baada ya serikali kutoa mwongozo
kwamba kila mlengwa wa vocha ya pembejeo lazima achukue mifuko miwili ya
minjingu mazao.
0 comments:
Post a Comment