Hapa Mr.LAITONI MWAKALINGA akionesha mkoano wake wa kulia nje ya ofisi za haki za binadamu wilayani Mbozi.(Picha na Mpiga picha wetu)
Na Mwandishi wetu.Mbozi.
Askari polisi saba wa kituo cha polisi
Mbozi wanatuhumiwa kwa kumpiga, kumjeruhi na kumsababishia maumivu makali
LAITON MWAKALINGA mwenye umri wa miaka 33 mkazi wa Kijiji cha Haterere.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na LAITON
MWAKALINGA alipigwa na askari wakati akipeleleka malalamiko dhidi ya shemeji
yake aliyemtishia kumuua ambapo askari hao walimtaka atoe kiasi cha shilingi elfu
arobaini na alipgoma ndipo walipoanza kumpiga hadi kumvunja mkono.
Kutokana na kitendo hicho Kamanda wa polisi
mkoani hapa DIWANI ATHUMANI ameahidi kulifuatilia tukio na kutoa wito kwa
wananchi kuendelea kutoa taarifa haraka na sahihi ili hatua za haraka za haraka ziweze kuchukuliwa.
Aidha Kamanda DIWANI amefanya juhudi za kukutana na LAITON MWAKALINGA ofisini kwake na moja ya ahadi aliyoitoa kwa Laiton ni kuhakikisha anapata matibabu ili aweze kuendelea na shughuli zake za kila siku.
Wakati huohuo amesema ni kosa kwa askari yeyote kumpiga raia hata kama amefanya kosa, na kwamba kutokana na kitendo walichofanya askari hao gwaride maalumu la utambuzi lilifanywa wilayani Mbozi na kuwabaini askari 7 kati ya 10 walibainika kuhusika na kitendo cha kumshambulia na kumuomba Rushwa ili waweze kwenda kumkamata mhalifu.
0 comments:
Post a Comment