Phillip Mangula |
MAKAMU
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara, Phillip Mangula ametoa
ruksa kwa wana CCM wanaotaka ubunge na udiwani katika majimbo na kata
zinazoshikiliwa na wapinzani kuanza kupitapita ili kutafuta ushawishi.
Wakati
akitoa ruksa hiyo, Mangula aliuliza “…Iringa tulishindwaje jimbo hili, alitokea
pepo gani, naomba mkemee pepo hao waliosababisha tushindwe ili 2015 tushinde
jimbo hili.”
Akihutubia
mamia ya wakazi wa mji wa Iringa na vitongoji vyake katika mkutano wake wa
kwanza alioufanya mjini hapa tangu ashike wadhifa huo, Mangula aliyekabidhi
kadi kwa wanachama wapya 171, alisema ruksa hiyo haihusu nafasi ya Rais na majimbo
na kata zinazoongozwa na wana CCM.
“Nimeambiwa
wapo walioanza kujenga makundi ndani ya chama kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu ujao.
Napenda kurudia tena ni marufuku kwa wanaCCM kuwabugudhi wanaCCM wenzao waliopo
madarakani,” alisema.
Katika
mkutano huo uliofanyika katika uwanja wa Mwembetogwa ukiwa na ulinzi mkali wa
Polisi, Mangula alisema wanaCCM wanaojipitisha kwenye maeneo yanayoongozwa na viongozi
wa CCM, wataenguliwa hata kama watashinda kura za maoni kwa ajili ya Uchaguzi
Mkuu wa 2015.
Alisema
kujipitisha katika maeneo wanayoyaongoza kunakibomoa chama hicho kwasababu ni
chanzo kikubwa cha makundi.
“Mgogoro
mkubwa ndani ya CCM ni makundi, makundi haya hujengwa kipindi cha kuelekea
uchaguzi, hayana la maana zaidi ya kutubomoa. Hivi sasa nimeambiwa wapo
walioanza kujenga makundi,” alisema.
Alisema
kwa kutumia kitengo chao cha kumbumbuku, watakusanya taarifa za wote
wanaowabughudhi wanaCCM wenzao waliopo madarakani ikiwa ni pamoja na nafasi ya
Rais na kuwashughulikia kabla ya uchaguzi mkuu ujao.
“Tutawaengua
sambamba na wale watakaobainika kutumia rushwa kutafuta uongozi. Tutafanya
hivyo kwa kuwa kanuni za maadili ya chama chetu zinatamka bayana kwamba ni
mwiko kwa mwanaCCM kutoa au kupokea rushwa,” Mangula alisema baada ya kumuomba
mwanahabari kusoma mbele ya mkutano huo kanuni inayopinga rushwa.
Baada
ta kuhitimisha mkutano huo majira ya saa 12.00 jioni, baadhi ya vijana
wanaodaiwa kuwa wafuasi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) walianza
fujo na kuuzomea msafara wa Mangula wakati ukitoka uwanjani hao.
Huku
wakizomea na wengine wakiimba kibwagizo cha ‘Peoples Power’ vijana hao walianza
kurusha mawe kabla askari Polisi waliokuwepo uwanjani hapo kuwadhibiti.
Wakati
vurugu hiyo ikiendelea mmoja wao aliyejitambulisha kwa Jacob Mosha alisema “Wanamchosha
tu mzee Mangula, hawezi kumudu jukwaa kwasababu sio mzungumzaji mzuri, badala
yake walipaswa kumrudisha kwenye nafasi yake ya utendaji.”
Kijana
huyo alisema sehemu kubwa ya hotuba ya kiongozi huyo ilitawaliwa na hoja
zilizopaswa kujadiliwa katika vikao vya ndani vya chama hicho.
“Wananchi
waliokuja kwenye mkutano huu walitaka kusikia kutoka kwake, nini CCM inataka
kufanya ili kukabiliana na kero nyingi zinazowakabili watanzania ikiwa ni
pamoja na ukosefu wa ajira kwa vijana wanaomaliza vyuo vikuu huku wakikabiliwa
na mikopo ya kusoma elimu hiyo” alisema.
“Badala
yake hotuba ya kiongozi huyo ilijaa maelekezo kwa wanaCCM wenzake ikizungumzia makundi
ndani ya chama, kanuni na adhabu kwa wanaoshindwa kuzingatia katiba na miongozo
mingine ya chama,” alisema.
Alisema
kitendo cha kiongozi huyo kuwaita ‘pepo’ wananchi waliokinyima kura katika
uchaguzi mkuu uliopita kinawaongezea hasira kwasababu kosa walilifanya wao
wenyewe.
“Lilikuwa
kosa lao, tena la kiufundi kweli kweli, na likawagharimu, kwasababu wanaCCM
walimtaka Frederick Mwakalebela aliyeshinda kura za maoni, lakini wao wakampa
Monica Mbega,” alisema.
Alisema
yeye alikuwa mmoja wa waliochukizwa na uamuzi wa CCM wa kumuengua Mwakalebela
na hivyo kura yake kumpigia Mchungaji Peter Msigwa wa Chadema ambaye baadaye
aliibuka mshindi katika jimbo hilo.
0 comments:
Post a Comment