Pages

Home » » MTWARA DAMU YA WATU SABA YAMWAGIKA NYUMBA ZA WABUNGE ZACHOMWA MOTO

MTWARA DAMU YA WATU SABA YAMWAGIKA NYUMBA ZA WABUNGE ZACHOMWA MOTO


Nyumba  za  wabunge zikiteketea kwa moto
watuhumiwa wa vurugu wakikamatwa
nyumba  za wabunge  zilizochomwa  moto leo

Na Abdulaziz Video Lindi

WATU saba akiwemo askari  polisi mmoja  wameuwawa huku  wengine  wakijeruhiwa  vibara katika vurugu  kubwa  zilizoibuka Mtwara mkoani Lindi

mbali ya watu hao  kuuwawa  pia Hosteli ya wanafunzi wa chuo cha Utumishi kilichoko manispaa yaMtwara/Mikindani  yakoswa koswa kuchomwa moto  hii leo kwa kilekinachodhaniwa kuwa na uhusiano na Hawa Ghasia pamoja na kituo kidogocha Polisi Cha Shangani mkoani Mtwara

Vurugu hizo zilizoanza leo  zimehamia wilayani Masasi mkoani
Mtwara ambapo Inasemekana Askari mmoja wa Upelelezi wa jeshi la Polisi

Ameuawa baada ya kujiingiza katika kundi na kubainika akiwapiga picha ambapo pia alikutwa na bastola 2 huku  Nyumba ya Mbunge wa Masasi(Mama Kasembe),Vifaa vya Mahakama ya mwanzo pamoja na magari ya Halmashauri nayo yateketezwa kwa Moto mchana hii leo katika vurugu za waandamanaji zilizoanza kwa waendesha Bodaboda kuanza kuandamana POLISI wakizidiwa na kulazimika kupiga mabomu ya machozi na risasi za moto ,

Taarifa za ambazo hazijathibitishwa na Mamlaka yeyote hadi hivi sasa
kufuatia simu za mkonononi za viongozi wa polisi kutopokelewa  ni
kwamba wananchi wanaendelea kufanya uharibifu mkubwa huko ambapo Polisi wamezidiwa na wamejifungia kituoni wanarusha mabomu yao tokea huko walikojificha maana nje hakutamaniki.
Na wameshateketeza nyumba ya mama Kassembe,Mbunge wa Masasi

Kikao cha dharura cha kamati ya ulinzi na usalama kinaendelea kwa
kuwashirikisha maafisa wa polisi na maafisa usalama waliotoka Dar es Salaam kuongezea nguvu. Maaskari na makachero wamewasili  Mtwara leo asubuhi na helkopta kuongezea nguvu.

Maandamano hayo ya Vurugu yalioongozwa na Madereva wa boda boda. Risasi za moto na mabomu ya machozi yanapigwa kutawanya watu na tayari nyumba moja imechomwa moto na baadhi ya magari huku Vijana wakizidi kusonga mbele
Jika Anda menyukai Artikel di blog ini, Silahkan klik disini untuk berlangganan gratis via email, dengan begitu Anda akan mendapat kiriman artikel setiap ada artikel yang terbit di Creating Website

0 comments:

Post a Comment

 
Support : Greyson Salufu | Chimbuko Letu Inc | Chimbuko Letu Inc
Copyright © 2011. Mbwile Media - All Rights Reserved
Template Modify by Chimbuko Letu Inc
Proudly powered by Blogger