Pages

Home » » PHILLIP MANGULA ATOA RUKSWA KWA WANACCM WANAOTOKA MAJIMBO NA KATA ZINAZOONGOZWA NA WAPINZANI KUANZA KUJIPANGA KWA UCHAGUZI WA 2015

PHILLIP MANGULA ATOA RUKSWA KWA WANACCM WANAOTOKA MAJIMBO NA KATA ZINAZOONGOZWA NA WAPINZANI KUANZA KUJIPANGA KWA UCHAGUZI WA 2015

Phillip Mangula
 MAKAMU Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara, Phillip Mangula ametoa ruksa kwa wana CCM wanaotaka ubunge na udiwani katika majimbo na kata zinazoshikiliwa na wapinzani kuanza kupitapita ili kutafuta ushawishi.
Wakati akitoa ruksa hiyo, Mangula aliuliza “…Iringa tulishindwaje jimbo hili, alitokea pepo gani, naomba mkemee pepo hao waliosababisha tushindwe ili 2015 tushinde jimbo hili.”
Akihutubia mamia ya wakazi wa mji wa Iringa na vitongoji vyake katika mkutano wake wa kwanza alioufanya mjini hapa tangu ashike wadhifa huo, Mangula aliyekabidhi kadi kwa wanachama wapya 171, alisema ruksa hiyo haihusu nafasi ya Rais na majimbo na kata zinazoongozwa na wana CCM.
“Nimeambiwa wapo walioanza kujenga makundi ndani ya chama kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu ujao. Napenda kurudia tena ni marufuku kwa wanaCCM kuwabugudhi wanaCCM wenzao waliopo madarakani,” alisema.
Katika mkutano huo uliofanyika katika uwanja wa Mwembetogwa ukiwa na ulinzi mkali wa Polisi, Mangula alisema wanaCCM wanaojipitisha kwenye maeneo yanayoongozwa na viongozi wa CCM, wataenguliwa hata kama watashinda kura za maoni kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu wa 2015.
Alisema kujipitisha katika maeneo wanayoyaongoza kunakibomoa chama hicho kwasababu ni chanzo kikubwa cha makundi.
“Mgogoro mkubwa ndani ya CCM ni makundi, makundi haya hujengwa kipindi cha kuelekea uchaguzi, hayana la maana zaidi ya kutubomoa. Hivi sasa nimeambiwa wapo walioanza kujenga makundi,” alisema.
Alisema kwa kutumia kitengo chao cha kumbumbuku, watakusanya taarifa za wote wanaowabughudhi wanaCCM wenzao waliopo madarakani ikiwa ni pamoja na nafasi ya Rais na kuwashughulikia kabla ya uchaguzi mkuu ujao.
“Tutawaengua sambamba na wale watakaobainika kutumia rushwa kutafuta uongozi. Tutafanya hivyo kwa kuwa kanuni za maadili ya chama chetu zinatamka bayana kwamba ni mwiko kwa mwanaCCM kutoa au kupokea rushwa,” Mangula alisema baada ya kumuomba mwanahabari kusoma mbele ya mkutano huo kanuni inayopinga rushwa.
Baada ta kuhitimisha mkutano huo majira ya saa 12.00 jioni, baadhi ya vijana wanaodaiwa kuwa wafuasi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) walianza fujo na kuuzomea msafara wa Mangula wakati ukitoka uwanjani hao.
Huku wakizomea na wengine wakiimba kibwagizo cha ‘Peoples Power’ vijana hao walianza kurusha mawe kabla askari Polisi waliokuwepo uwanjani hapo kuwadhibiti.
Wakati vurugu hiyo ikiendelea mmoja wao aliyejitambulisha kwa Jacob Mosha alisema “Wanamchosha tu mzee Mangula, hawezi kumudu jukwaa kwasababu sio mzungumzaji mzuri, badala yake walipaswa kumrudisha kwenye nafasi yake ya utendaji.”
Kijana huyo alisema sehemu kubwa ya hotuba ya kiongozi huyo ilitawaliwa na hoja zilizopaswa kujadiliwa katika vikao vya ndani vya chama hicho.
“Wananchi waliokuja kwenye mkutano huu walitaka kusikia kutoka kwake, nini CCM inataka kufanya ili kukabiliana na kero nyingi zinazowakabili watanzania ikiwa ni pamoja na ukosefu wa ajira kwa vijana wanaomaliza vyuo vikuu huku wakikabiliwa na mikopo ya kusoma elimu hiyo” alisema.
“Badala yake hotuba ya kiongozi huyo ilijaa maelekezo kwa wanaCCM wenzake ikizungumzia makundi ndani ya chama, kanuni na adhabu kwa wanaoshindwa kuzingatia katiba na miongozo mingine ya chama,” alisema.
Alisema kitendo cha kiongozi huyo kuwaita ‘pepo’ wananchi waliokinyima kura katika uchaguzi mkuu uliopita kinawaongezea hasira kwasababu kosa walilifanya wao wenyewe.
“Lilikuwa kosa lao, tena la kiufundi kweli kweli, na likawagharimu, kwasababu wanaCCM walimtaka Frederick Mwakalebela aliyeshinda kura za maoni, lakini wao wakampa Monica Mbega,” alisema.
Alisema yeye alikuwa mmoja wa waliochukizwa na uamuzi wa CCM wa kumuengua Mwakalebela na hivyo kura yake kumpigia Mchungaji Peter Msigwa wa Chadema ambaye baadaye aliibuka mshindi katika jimbo hilo.
Jika Anda menyukai Artikel di blog ini, Silahkan klik disini untuk berlangganan gratis via email, dengan begitu Anda akan mendapat kiriman artikel setiap ada artikel yang terbit di Creating Website

0 comments:

Post a Comment

 
Support : Greyson Salufu | Chimbuko Letu Inc | Chimbuko Letu Inc
Copyright © 2011. Mbwile Media - All Rights Reserved
Template Modify by Chimbuko Letu Inc
Proudly powered by Blogger