Timu ya Young Africans Sports Club yenye makao makuu
yake jijini Dar es salaam nchini Tanzania siku ya jumamosi itashuka dimbani
kucheza mchezo wa kirafiki na timu ya Arminia Bielefeld ya kutoka nchini
Ujerumani, mchezo utakaofanyika katika mji wa Antalya.
Young Africans ambayo imeweka kambi
ya mafunzo jijini Antalya itatumia mchezo huo kama fursa pekee ya kuweza kujipima
uwezo dhidi ya timu hiyo ya Ujerumani ambayo pia imekuja kambi y amafunzo
kujiandaa na mzunguko wa ligi daraja la pili nchini Ujerumani.
Kocha Mkuu wa Young Africans Ernest
Brandts amesema kwao ni furaha kwa kupata nafasi ya kucheza na timu kubwa kama
ya Armini Bielefeld ambayo inawachezaji wa kiwango cha kimataifa hivyo anaamini
utakua ni mchezo safi na kuwavutia.
Unajua tun siku sita (5) tangu
tufike hapa mjini Antalya Uturuki na tumeshafanya mazoezi kwa siku nne
(4) hivo fursa ya kupata mchezo wa kirafiki ni nzuri sana kwetu kwani itanipa
nafasi ya kuona wachezaji wangu wameshayashika kwa kiasi gani mafunzo yangu
alisema 'Brandts'
Arminia Bielefeld imeshawasili
mjini Antalya kwa ajili ya kambi yake ya mafunzo na hivyo kwao pia ni fursa nzuri
ya kuweza kujipima uwezo na timu ya Young Africans ambao ni mabingwa mara 23
katika ligi kuu ya Tanzania.
Leo asubuhi Young Africans
imeendelea na mazoezi katika viwanja wa Fame Residecne tayari kabisa kujiandaa
na mchezo huo utakaochezwa siku ya jumamosi mjini Antalya.
Kikosi cha wachezaji 27 waliopo
mjini Antalya wote wako katika hali nzuri na hakuna maheruhi hata mmoja hali
itakayompa kocha Brandts kuamua kumtumia mchezaji yoyote katika mchezo huo.
0 comments:
Post a Comment