JUKWAA
la Katiba Tanzania (JUKITA) limesema kuwa katika muongozo wa Tume juu
ya muundo na utaratibu wa kupata wajumbe wa mabaraza ya Katiba ya Wilaya
na Asasi unamapungufu katika baadhi ya vipengele .
Akizungumza Dar es Salaam leo Mwenyekiti wa Jukwaa la Katiba Tanzania Deus Kibamba
alitaja baadhi ya mapungufu hayo kuwa ni Madiwani wasiwe wajumbe wa
moja kwa moja wa Mabaraza ya Katiba ya Wilaya,maoni juu ya mwongozo
yametolewa na watu wachache,sifa za watakaochaguliwa kuwa wajumbe wa
mabaraza ya katiba ya wilaya zinamapungufu.
Deus
alisema ili kupanua wigo wa Demokrasia na kuepuka mgongano wa kimaslahi
,Jukwaa limependekeza kuwa Madiwani wasiei wajumbe wa moja kwa moja kwa
nyadhifa zo,katika mabaraza ya Wilaya ,Ngazi ay Serikali za Mitaa na
badala yake wanaotaka kuwa wajumbe wajumbe waombe ridhaa mpya ya
wananchi ili kuweza kuchaguliwa katika mabaraza hayo.
Alisema
kuwa sababu za kutoa mapendekezo hayo kuwa madiwani wasingie kwa nafasi
zao kwasababu Madiwani walichaguliwa kwa ajili ya kazi ya kuwawakilisha
wananchi katika ngazi ya mabaraza ya Madiwani ya Wilaya ,manispaa ,miji
na majiji na si kwa ajili ya mabaraza ya katiba.
Alieleza
wawakilishi wanne watakaochaguliwa kutoka kila kijiji na kata watakuwa
na mamlaka stahili ya kuwakilisha wananchi kama ilivyo kwa madiwani
katika mabaraza ya madiwani.
Alifafanua
kuwa uwakilishi wa madiwani utaleta mgongano wa itikadi za vyama
vilivyowaweka madiwani hao madarakani hivyo kuleta msigano kwenye
mchakato wa mabaraza ya katiba.
‘’kama
kuna ulazima wa madiwani kuingia katika mabaraza hayo madiwani husika
waombe ridhaa ya kuingia katika mabarza kwa kupigiwa kura kupitia kijiji
husika’’alisema Deus
Aidha
alisema kuingia kwao moja kwa moja kutaweka mazoea mabaya kwa vyombo
vitavyoundwa siku za badae katika mchakato huo wa katiba mpya pamoaj na
kuingia kwao kunaleta utata juu ya endapo wabunge ambao nao ni madiwani
kwa nyadhifa zao kama wabunge ,watashiriki mabaraza ya katiba au
hawatashiriki .
Sababu
nyingine kuwa madiwani jukumu lao ni usimamamizi wa shughuli za
maendeleo na masuala ya uongozi na siasa katika kila kata hivyo
wanashauriwa madiwani wabaki hivyo ili wasaidie wanapohitaji ka katika
majukumu hayo ya kila siku kuliko wakiwa wajumbe katika mabaraza ya
katiba.
Alisema
walibaini kuwa muongozo unatoa madaraka yasiyo na ukomo kwa watendaji
wa vijiji na masheha katika kuratibu zoezi la upatikanaji wa wajumbe wa
mabaraza ya katiba.
Alisema
Pamoja na mapendekezo hayo muongozo utamke bayaana namana madaraka hayo
yanavyodhibitiwa kwa kutamka watu wanaoweza kumzuia asiweke upendeleo
kwa baadhi ay watu waliopendekezwa kuwa wajumbe wa mabaraza ya katiba.
Hatahivyo alisema endapo mapungufu aytafanyiwa kazi Muongozo huo utakuwa ni mfano wa kuigwa na utafanya kazi ya mabaraza ya katiba yawe ya wazi na shirikishi kwa kiwango kikubwa.
0 comments:
Post a Comment