Mchezaji
wa timu ya Azam FC Kipre Cheche akiwania mpira katikati ya wachezaji
Ladu Manas kulia na Joseph Odongi wa timu ya El Nasir FC ya Sudan
Kusini katika michuano ya Kombe la Shirikisho uliochezwa kwenye uwanja
wa Taifa jijini Dar es salaam jioni hii, Timu ya Azam imeibuka na
ushindi wa magoli 3-1 ambapo wafungaji wa Mgoli hayo ni Abdi Kassim,
Kipre Cheche na John Boko wakati lile la timu ya El Nasir FC limefungwa
na mchezaji Fobian Elias, huu ni mwanzo mzuri wa timu ya Azam FC ambapo
timu hizo zitarudiana wiki mbili zijazo nchini Sudan Kusini.
Mchezaji
wa timu ya Azam FC Abdi Kassim akipiga mpira wa kichwa na kufunga goli
la kwanza mbele ya mchezaji wa timu ya El Nasir FC Simon Amaya.
Mchezaji
Abdi Kasim akishangilia kwa kusujudu mara baada ya kufunga goli la
kwanza kwa timu yake huku wachezaji wenzake wakimuangalia.
Kikosi cha timu ya El Nasir FC ya Sudan Kusini kikiwa katika picha ya pamoja kabla ya kuanza kwa mchezo huo.
Kikosi cha timu ya Azam FC kikiwa katika picha ya pamoja kabla ya kuanza kwa mchezo huo.
Wachezaji wakisalimiana
Wachezaji wakiingia uwanjani tayari kwa mpambano huo jioni hii katika uwanja wa Taifa.
0 comments:
Post a Comment