Pages

Home » » MGAMBO WAKIPOKEA KICHAPO KWA KUSIMAMIA SHERIA IRINGA

MGAMBO WAKIPOKEA KICHAPO KWA KUSIMAMIA SHERIA IRINGA


Wananchi  wa Manispaa ya Iringa  wakishuhudia ugomvi kati ya mgambo  wa Manispaa ya Iringa na kijana aliyekutwa akivunja sheria ya usafi kwa  kujisaidia ovyo leo (picha zote na Denis Mlowe)
Hapa mgambo  wa manispaa ya Iringa kushoto na kulia  wakililazimisha jemba hilo katikati  kuingia ndani ya geti la Manispaa ya Iringa japo jitihada hazikuzaaa matunda
Hapa jemba  hilo kulia  likijipanga kuanza kutoa dozi ya kichapo kwa mgambo
Hapa jemba hilo likipandisha midadi ili kuanza  kutembeza kichapo  kiasi cha mgambo hao  kuanza kutoa heshima "shikamoo kaka"
Hapa  wananchi  wakisaidia kumwokoa mchafuzi  huyo wa mazingira

Hapa njemba  hilo  likiondoka kitemi  huku  wananchi  wakishangilia
kazi  ilikuwa  hivi njemba  hilo kushoto likimkwida  mmoja kati ya mgambo wa Manispaa huku msamaria mwema kulia akisaidia na huyo ndio mgambo aliyezimishwa kwa ngumi
hapa mgambo akitimu mbio mbio  huku njemba  hilo  likiwafuata kwa nyuma  baada ya  kushinda vita 

 Habari ni Francis Godwin
 Pamoja na Halmashauri ya Manispaa ya Iringa kuweka sheria ya kuwabana wanaochafua mji huo kwa kujisaidia ovyo ama kutupa taka kwa kuwatoza faini ya shilingi 50,000 wavunjaji wa sheria hao , leo mgambo wa Manispaa hiyo wamejikuta wakipokea kichapo kutoka kwa mjenda mmoja ambae alikuwa akijisaidia haja ndogo .
 Tukio hilo limetokea mida ya saa 6 mchana nje ya uzio wa Manispaa ya Iringa baada ya mgambo wa Manispaa hiyo kumkamata kijana mmoja aliyevalia mavazi ya mgambo a.k.a mjeda kushindwa kuvumilia kuvunjiwa heshima na mgambo kwa kutozwa faini na kuamua kutembeza kichapo.
Vurugu hizo zimesababisha mmoja kati ya mgambo kujeruhiwa kwa kupigwa ngumi katika paji lake la uso na jichoni na hivyo kupelekea mgambo hao kutimua mbio kuhofia madhara makubwa zaidi.
Katika tukio hilo ambalo lilikusanya umati wa wananchi ambao walionekana kushuhudia burudani hiyo ya ngumi limechukuliwa kwa mtazamo tofauti na wananchi hao huku baadhi yao wakisifu mgambo hao wa Manispaa kwa kusimamia vema sheria na wengine wakimlalamikia mvunja sheria huyo kwa kujisaidia ovyo.
Hata hivyo sheria ya Manispaa ya Iringa mbali ya kuwekwa ila bado baadhi ya wananchi wameendelea kuvunja kwa kujisaidia ovyo jambo ambalo bado linahitaji jitihada zaidi katika kuboresha mji wa Iringa.
Jika Anda menyukai Artikel di blog ini, Silahkan klik disini untuk berlangganan gratis via email, dengan begitu Anda akan mendapat kiriman artikel setiap ada artikel yang terbit di Creating Website

0 comments:

Post a Comment

 
Support : Greyson Salufu | Chimbuko Letu Inc | Chimbuko Letu Inc
Copyright © 2011. Mbwile Media - All Rights Reserved
Template Modify by Chimbuko Letu Inc
Proudly powered by Blogger