mtoto zawadi Godfrey Mwingune mwenye siku 19 kama anavyoonekana akiwa
na macho matatu na uvimbe mkubwa katika paji lake la uso huku
kichwani kukiwa na nundu mfano wa uyoga ambayo inatoa usaa mwingi
Hivi ndivyo mtato zawadi anavyoonekana kichwa chake uzito wake ni
kg 4 na nusu alizaliwa hospitali ya kibena Njombe ni mwenyeji wa
Ikengeza Isimani mkoa wa Iringa
Hapa mtoto zawadi akiwa amejipumzisha katika kitanda
Na.Farnsis Godwin, Iringa.
Wazazi wa mtoto Zawadi Gofrey Mwingune Bw Godfrey Mwingune (30) na
mama wa mtoto huyo Mathar Kitago (28) wakimtazama mtoto wao kwa huzuni
mwingi kutokana na kukosa fedha za matibabu kwa ajili ya kumsafirisha
mtoto huyo kwenda kufanyiwa upasuaji katika Hospitali ya Taifa
HUJAFA hujaumbika ,Mungu ana makusudi yake ni yeye ni muweza wa yote
kwani ndie aliyeumba mbingu na nchi pamoja na viumbe wote
wasioonekana na wanaoonekana hivyo mwacheni Mungu aitwe Mungu,ni kauli
ya wazazi wa mtoto Zawadi Godfrey Mwingune aliyezaliwa akiwa na macho
matatu na kichwa mfano wa uyoga.
Akizungumza na mwandishi wa habari hii mama
mzazi wa mtoto Zawadi Bi .Mathar Kitago (28) mzaliwa wa kijiji cha
Kidegembye Lupembe wilayani Njombe mkoani Njombe alisema kuwa hadi
sasa anamwachia Mungu ambae ndie amempa zawadi ya mtoto huyo.
Kwani amesema kuwa ilikuwa ni siku ya jumapili January 13 mwaka huu
aliposhikwa na uchungu na kukimbizwa katika kituo cha afya cha
Kidegembye ambako alichukuliwa na kukimbizwa Hospitali ya wilaya ya
Njombe Kibena kwa matibabu zaidi.
Hata hivyo alisema baada ya kufika katika Hospitali hiyo aliingizwa
katika chumba cha upasuaji na kufanyiwa upasuaji na kubahatika kupata
mtoto huyo japo kwa upande wake aliogopa sana baada ya kuonyeshwa
mtoto huyo ila alipiga moyo konde kwa kuwa ni damu yake .
Bi Mathar mwenye idadi ya watoto watatu sasa akiwemo Zawadi
anasema kuwa mtoto wa kwanza wa kiume ana miaka 9 na mtoto wa pili
ni wa kike ana miaka 4 na wote alijifungua vizuri bila kufanyiwa
upasuaji kama ilivyotokea kwa mtoto Zawadi.
Baba wa mtoto huyo Bw Godfrey Mwingune ambae anategemea kuendesha
maisha yake kwa kilimo anasema kuwa yeye ni mzaliwa wa kijiji cha
Ikengeza Isimani na kuwa baada ya kupata mtoto huyo wa ajabu aliamua
kurejea nyumbani kwa wazazi wake Igengeza Ismani ili kuwaonyesha
mtoto huyo japo anatambua kuwa mtoto huyo ni zawadi kutoka kwa Mungu
na ndio sababu ya kumpata jina la Zawadi pia.
" Kweli nilipomleta kwa wazazi kijijini nao wamebaki wakishangaa
kuona mtoto wa ajabu hivyo ila sasa tunafanyaje yote ni mipango ya
Mungu "
Mwingune alisema kuwa hali ya afya ya mtoto huyo si nzuri kwani mbali
ya kuzawali wa kilo 4 na nusu ila bado anatatizo la uvimbe katika paji
lake la uso pia kichwani kuna kovu kubwa ambalo ni kama ncha mbili hivi
ambalo linatoa usaa mwingi na kuwa jeraha hilo alizaliwa nalo mbali
na vituko hivyo pia alisema katika jicho lake la kushoto kwa juu
kuna jicho la pili na kufanya mtoto huyo kuwa na macho matatu .
Alisema kuwa tayari mtoto huyo amepata kutibiwa Hospitali ya
Kibena Njombe na Hospitali ya Rufaa Mbeya ila imeshindikana na
madaktari wamemtaka amkimbize katika Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa
matibabu zaidi ama nje ya Tanzania .
Hata hivyo mzazi huyo anasema kuwa kwa sasa pesa ya haraka
inayohitajika ni kiasi cha Tsh. milioni 1.5 ili kumwezesha kwenda
kuanza matibabu Muhimbili japo gharama za matibabu zinaweza
kuongezeka zaidi wakati kwa upande wake hana uwezo wa kupata hata
shilingi 100,000 na kuwapongeza wakazi wa Isimani ambao wamemchangia
kiasi cha shilingi 300,000.
0 comments:
Post a Comment