Rais
Mstaafu Mzee Ali Hassan Mwinyi akimkabidhi tuzo Shomari Kapombe
mwanamichezo bora wa Mwaka 2012 katika sgerehe zilizofanyika kwenye
ukumbi wa Diamond Jubelee mwaka jana katikati ni mmoja wa maofisa
waandamizi wa TASWA.
………………………………………………..
TUZO za Wanamichezo Bora
wa Tanzania wa mwaka 2013 zinazoandaliwa na Chama cha Waandishi wa
Habari za Michezo Tanzania (TASWA) zitafanyika Aprili 27 mwaka huu
jijini Dar es Salaam.
Kamati inayoratibu tuzo hiyo
ilifanya kikao chake cha kwanza Jumanne wiki hii, ambapo wajumbe wa
kamati hiyo walikubaliana mambo mbalimbali ya kimsingi kuhakikisha tuzo
zinakuwa na mvuto kama ilivyokuwa miaka iliyopita na pengine ziwe bora
zaidi.
Kutokana na hali hiyo vyama vyote
vya michezo vilivyosajiliwa na Baraza la Michezo la Taifa (BMT),
ambavyo vipo hai na vinaendesha mashindano vitaandikiwa barua kwa ajili
ya kutoa mependekezo yao ya wanamichezo waliofanya vizuri kwa mwaka jana
upande wa michezo yao na yawasilishwe kabla ya Februari 28, mwaka huu.
Tunaomba ieleweke kuwa vyama
vitatoa mapendekezo na hivi sasa Kamati ya Tuzo inafanya mazungumzo na
kampuni mbalimbali zinazohusika na mambo ya mawasiliano ili kuona namna
zitakavyoshirikiana na wadau katika kuchambua majina hayo, ambapo kila
chama kimetakiwa kiwasilishe majina matano ya wanamichezo wao kwa kila
jinsia kama ni mchezo unaochezwa na jinsia mbili, lakini kama ni mchezo
wa jinsia moja watatakiwa kuwasilisha majina matano ya jinsia husika tu.
Yapo marekebisho kadhaa
yamefanyika ikiwa ni pamoja na kuongeza idadi ya tuzo kutoka 36 za mwaka
jana hadi kufikia 42 mwaka huu na idadi inaweza kuongezeka ama kupungua
kulingana na sifa za wanamichezo ambazo vyama vitaleta.
Tunaomba wadau watupe ushirikiano
wa kutosha katika jambo hili ili kuzifanya tuzo ziwe bora na
kuhakikisha kila anayestahili kupata tuzo anazawadiwa kwa kuthamini kile
alichokifanya, ambapo ukumbi utakapofanyika tuzo hizo utatangazwa hivi
karibuni baada ya kukamilisha baadhi ya mambo.
Idadi ya michezo itakayopewa tuzo
pamoja na aina nyingine ya tuzo zitakazotolewa ikiwemo Tuzo ya Heshima
tutaendelea kujulishana kadri siku zitakavyokuwa zinasonga mbele.
Washindi wa kila tuzo ndiyo mmojawapo ataibuka kuwa Mwanamichezo Bora wa
Tanzania Mwaka 2012.
Dhamira ya kamati yangu ni kutaka
kuhakikisha kuwa TASWA haikukosea kututeua na tutaleta wanammichezo
sahihi na hatimaye kumpata yule bora ambaye ataungana na wengine
waliopata kutwaa tuzo hiyo miaka ya nyuma.
Wanamichezo ambao wamepata kutwaa
Tuzo ya Mwanamichezo Bora Mwaka wa Tanzania ni Samson Ramadhan (2006),
Martin Sulle (2007) na Mary Naali (2008) wote wakiwa wanariadha, wakati
mwaka 2009 alikuwa Mwanaidi Hassan na mwaka 2010 alikuwa pia Mwanaidi
Hassan ambaye ni mcheza netiboli na mwaka 2011 alikuwa mwanasoka Shomari
Kapombe.
0 comments:
Post a Comment