Sheikh
Hasani Kabeke wa Mwanza akichangia katika kikao cha klutatafuta
muafaka kati ya Waislamu na Wakristo kuhusu uchanjaji wanyama
kilichoitishwa na Waziri Mkuu Mizengo Pinda kwenye ukumbi wa Banki Kuu
jijini Mwanza Februari 16, 2013.(Picha na Ofisi yaWaziri Mkuu)
Viongozi
wa madhehebu ya Dini ya Kikristo wakimsikiliza Waziri Mkuu, Mizengo
Pinda wakati alipozungumza na Viongozi wa Dini ya Kiislam na Kikristo
kujadili mgogoro wa uchinjaji wanyama kwenye ukumbi wa Benki Kuu jijini
Mwanza Februari 16,2013. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Viongozi
wa madhehebu ya Dini ya Kiislam wakimsikiliza Waziri Mkuu, Mizengo
Pinda wakati alipozungumza na Viongozi wa Dini ya Kiislam na Kikristo
kujadili mgogoro wa uchinjaji wanyama kwenye ukumbi wa Benki Kuu jijini
Mwanza Februari 16,2013. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Mkurugenzi
wa Radio ya Kikristo ya jijini Mwanza ya Kwaneema, Askofu Mpemba
akichangia katika kikao kati ya Waziri Mkuu Mizengo Pinda na Viongozi wa
dini za Kikristo na Dini ya Kiislamu cha kujadili mgogoro wa uchinjaji
wanyama kilichofanyika kwenye ukumbi wa Benki Kuu jijini Mwanza
Februari 16,2013.(Picha na Ofisi yaWaziri Mkuu)
Waziri Mkuu Mizengo Pinda akizungumza na Mkurugenzi wa Radio ya Kikristo ya jijini Mwanza ya Kwaneema, Askofu Mpemba.
Waziri
Mkuu, Mizengo Pinda kijadili jambo na Sheikh Mkuu wa Wilaya ya
Sengerema, Ahmed Ali (kushoto) na Sheikh wa msikiti wa Buswelu,
Athumani Ali katika kikao cha kujadili mgogoro wa uchinjaji wanyama
kati ya Waziri Mkuu na viongozi wa dini za Kikristo na Kiislamu
kilichofanyika kwenye ukumbi wa Benki kuu jijini Mwanza Februari 16,
2013. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
………………………………………………………………….
Na Frederick Katulanda
SAKATA la nani achinje nyama kati
ya Waislamu na Wakristo bado linaumiza vichwa, ambapo Waziri Mkuu,
Mizengo Pinda amesema mazoea ya tangu zama za kale yanayowaruhusu
Waislamu kuchinja nyama yaendelee, hadi hapo maamuzi mengine
yatapofikiwa na Serikali.
Kufuatia hali hiyo, Pinda
ameagiza kuundwa kamati maalumu itakayohusisha pande zote mbili za
Waislamu na Wakiristo, ambayo itashughulikia mgogoro huo, na kwamba kazi
hiyo ifanyike haraka iwezekanavyo, na kisha ripoti yake iwasilishwe
Serikalini kwa hatua zaidi za kimaamuzi.
Waziri Pinda ameyasema hayo muda
mfupi uliopita leo, wakati akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari,
kuhusiana na kikao chake cha pamoja na viongozi wa Kikristo na Kiislamu,
kilichofanyika katika ukumbi wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), tawi la
Mwanza, kwa lengo la kutatua mgogoro wa kidini unaoonekana kuota mizizi.
Kauli hiyo ya Waziri Mkuu Pinda,
imekuja siku chache baada ya kutokea mapigano makali baina ya wafuasi wa
dini ya Kiislamu na Wakiristo kuzuka huko Buseresere-Katoro katika
Wilaya ya Chato mkoani Geita, ambapo mchingaji mmoja aliuawa kwa
kuchinjwa huku watu wengine kadhaa wakijeruhiwa vibaya.
Aidha, Pinda alikemea vikali
vurugu za kidini zilizotokea mkoani Geita, na kuwataka viongozi wa
madhehebu yote ya dini kuheshimiana, kujenga mshikamano na
kutohasimiana, kwani wao ni watu muhimu sana katika maendeleo na utulivu
wa nchi.
0 comments:
Post a Comment