Watu
watano wamefariki dunia kwa kupigwa na radi leo katika wilaya za Mbozi na
Mbarali mkoani Mbeya baada ya mvua kubwa iliyoambatana na radi ya mara kwa mara.
Katika
tukio hilo watu watatu wa familia moja akiwemo mama na watoto wake wawili wakazi
kitongoji cha mpanda kati Kata ya Nyimbili wamefariki dunia baada ya kupigwa na
radi leo wakati mvua ikiendelea kunyeesha majira ya saa saba za mchana.
Waliofariki
ni JERUMANA KUMI HALINGA mwenye umri wa miaka 35, DAVID HALINGA mwenye umri wa
miaka 5, KUMI HALINGA mwenye umri wa miaka 3 na kumjeruhi mtoto wa miezi 9 ambaye
amekimbizwa katika katika zahanati ya kata ya Nyimbili.
Tukio
la pili limetokea katika kijiji cha Magurula kata ya Utengule Usangu ambapo KASIM
SAGUTANGU amefariki dunia kwa kupigwa na radi baada ya kunyesha mvua kubwa
Februari 3 mwaka huu majira ya saa nane za mchana
Matukio
yote hayo yamethibitishwa na maafisa watendaji wa vijijini hivyo ambapo kwa
tukio la Mbozi limethibitishwa na mtendaji wa kijiji LEMSI NZOWA.
Aidha tukio jingine limetokea katika kijiji cha Mbagala kata ya Ilembo ambapo mke wa mchungaji wa kanisa la Moravian ushirika wa Kesaria Mch.MAGANGA aliyefahamika kwa KOTANIDA PETRO AU MAMA ALFA amefariki dunia baada ya kupigwa na radi akiwa shambani kwake.
Mganga mfawidhi wa Kituo cha afya cha Ilembo Dakta NELSON JOJI amekiri kupokea mwili huo na kusema kuwa uchunguzi umekamilika.

Kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya DIWANI ATHUMANI amethibitisha kutokea kwa matukio hayo yote.
0 comments:
Post a Comment