MOJA YA MTOTO MAJERUHI AKIHAMISHWA KUTOKA KATIKA HOSPITALI YA MISION CHIMARA NA KUPELEKWA HOSPITALI YA RUFAA MBEYA |
MOJA YA MAJERUHI AKISUBIRI KUPATA MATIBABU |
HILI NDILO ROLI WALIMOPANDA VIBARUA HAO WA SHAMBA LA KAPUNGA |
KWELI MUNGU NI MKUU HUWALINDA WATOTO WADOGO HAPA MKUU WA MKOA AKIMPA MOJA YA WATOTO WALIOPATA AJALI |
HUYU BINTI NI MWANAFUNZI NAE ALIKUWEPO KWENYE AJALI HIYO |
MKUU WA MKOA MBEYA ABAS KANDORO AKIONGEA NA WAANDISHI WA HABARI |
HAWA WOTE NI WANAFUNZI WALIKUWA WANAENDA KUFANYA KIBARUA CHA KULIMA KWA MWEKEZAJI KATIKA SHAMBA HILO LA KAPUNGA |
MAJERUHI 22 WAKIPAKIZWA KATIKA ROLI AINA YA FUSO TAYARI KUPELEKWA KATIKA HOSPITALI YA RUFAA MBEYA |
MAJERUHI WAKISAFIRISHWA KWENDA MBEYA |
Mkuu wa mkoa wa Mbeya ABASI
KANDORO amekerwa na tabia ya watoto kuacha shule na kukimbilia kufanya kazi
kwenye mashamba ya mwekezaji wa shamba la Kapunga Rice Project.
Hali hiyo ameionesha mara
baada ya kutembelea majeruhi wa ajali ya lori aina ya Scania lenye namba za
usajili T.398 BSE kuacha njia na kupinduka kutokana na mwendeokasi uliochangiwa
na abiria waliokuwa kwenye gari hilo
Amesema kutokana kitendo hicho
cha watoto kuacha shule na kukimbilia kufanya kazi kwenye mashamba kinawanyima
haki zao, hivyo ameahidi kufuatilia ili kudhibi kitendo hicho.
Aidha
KANDORO amesema katika ajali hiyo watu watano wamefariki dunia ambapo kati yao
watatu wametambuliwa ambao ni SAMWELI MAPUGILO MBENA mwenye umri wa miaka 30
mkazi wa Ilembula, BON MFIPA mwenye umri miaka 27 mkazi wa mapogolo na EDGAR
MWAKIPESILE mwenye umri wa miaka 35 mkazi wa Nonde Mbeya huku mwanamke mmoja na
mwanaume bado hawajatambulika.
Kuhusu hatua za kuharakisha huduma za
afya kwa majeruhi hao Serikali imetuma madawa na madaktari katika hospitali ya
chimala ili kuongeza nguvu kwa wahudumu wa afya.
WILAYA YA
MBARALI - AJALI YA GARI KUPINDUKA NA KUSABABISHA VIFO NA MAJERUHI
MNAMO TAREHE 01/02/2013 MAJIRA YA SAA 07:15
HRS HUKO KAPUNGA CHIMALA WILAYA YA MBARALI MKOA WA MBEYA. GARI NAMBA T.398 BSE
SCANIA TIPPER 114 MODEL MALI YA MWEKEZAJI AITWAYE KAPUNGA RICE PROJECT
LIKIENDESHWA NA DEREVA AITWAYE BARAKA S/O MOLLEL , MIAKA 29,MMASAI NA MKAZI WA
MATEBETE LIKIWA LIMEBEBA VIBARUA WA KUPANDA MPUNGA KUTOKA KIJIJI CHA MAPOGORO
KWENDA KATIKA SHAMBA LA MWEKEZAJI. GARI HILO LIKIWA NDANI YA SHAMBA HILO LILIACHA
NJIANA KUPINDUKA KISHA KUSABABISHA VIFO VYA WATU WATATU [3] NA MAJERUHI KWA WATU 130 WATU WALIOFARIKI WAMETAMBULIWA 1. SAMWELI S/O MAPUGILO, MBENA, 30YRS NA
MKAZI WA ILEMBULA 2. BON S/O MFUPA,
MNYAKYUSA, 27 YRS MKAZI WA MAPOGOLO NA3.EDGAR
S/O MWAKIPESILE, MIAKA 35, KYUSA, MKULIMA MKAZI WA NONDE MBEYA.AIDHA KATIKA
AJALI HIYO WATU 130WALIJERUHIWA KATI
YAO WANAUME 89 NA WANAWAKE 41.MAJERUHI 74WAMEPELEKWA HOSPITALI YA MISHENI CHIMALA KWAAJILI YA MATIBABU KATI
YAO WANAUME 49 NA WANAWAKE 25NA MAJERUHI 56WAMEPELEKWA HOSPITALI YA RUFAA MBEYA KWA MATIBABU ZAIDI MIONGONI
MWAO WANAWAKE 16 NA WANAUME 40.CHANZO CHA AJALI NI MWENDO KASIULIOSABABISHWA
NA VIBARUA WALIOKUWA NDANI YA GARI HILO KUMSHANGILIA DEREVA NA GARI LILIPOFIKA KWENYE KONA LILIMSHINDA KUKATA
KONA NA KUPINDUKA.DEREVA ALIKIMBIA MARA BAADA YA TUKIO HILO. KAMANDA
WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI ANATOA WITO KWA MADEREVA KUWA MAKINI WAWAPO
BARABARANI KWA KUZINGATIA SHERIA ZA USALAMA BARABARANI ILI KUEPUSHA AJALI
ZINAZOWEZA KUEPUKIKA.AIDHA ANATOA WITO KWA MTU/WATU WENYE TAARIFA MAHALI ALIPO
DEREVA AZITOE ILI AKAMATWE VINGINEVYO AJISALIMISHE MARA MOJA. PIA ANAWAASA
WANANCHI KUACHA TABIA YA KUWASHABIKIA MADEREVA WANAOENDESHA VYOMBO VYA MOTO KWA
MWENDO KASI KWANI INAWEZA KUHATARISHA MAISHA NA MALI ZAO.
Signed
By,
[DIWANI
ATHUMANI - ACP]
KAMANDA
WA POLISI MKOA WA MBEYA.
0 comments:
Post a Comment