Pages

Home » » RPC MBEYA-UJAMBAZI HAUNA NAFASI TENA MBEYA, VIJANA WAJITUME KATIKA SHUGHULI ZA KIMAENDELEO AMBAZO NI HALALI NA ZILIZOHARALISHWA KISHERIA."AMESEMA HAYO BAADA YA JESHI LAKE KUWADHHIBITI WATU WATANO WANAOSADIKIWA KUWA NI MAJAMBAZI"

RPC MBEYA-UJAMBAZI HAUNA NAFASI TENA MBEYA, VIJANA WAJITUME KATIKA SHUGHULI ZA KIMAENDELEO AMBAZO NI HALALI NA ZILIZOHARALISHWA KISHERIA."AMESEMA HAYO BAADA YA JESHI LAKE KUWADHHIBITI WATU WATANO WANAOSADIKIWA KUWA NI MAJAMBAZI"


Baadhi ya wananchi wakitoka kutambua miili ya wanaodhaniwa kuwa ni majambazi

Tunaomba radhi kwa kuonyesha picha hizi kwani mpaka sasa maiti hizi hazijatambulika


Kamanda diwani akiwaonyesha moja ya jambazi lililokuwa limeshika siraha




Hii ndiyo Gari iliyotumiwa na majambazi hayo

Siraha walizokuwa wanatumia majambazi hayo


Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Diwani Athumani amewaambia Wandishi wa Habari Ofisini kwake kuwa Tukio hilo limetokea leo majira ya Sita Mchana katika kijiji cha Garijembe Wilaya ya Mbeya katika Barabara ya Mbeya Tukuyu.




Kamanda Diwani akikagua gari ya majambazi yaliouwawa


MTANDAO wa Ujambazi nchini hususani Mkoani Mbeya umezidi kusambaratishwa  baada ya watu watano wanaodahaniwa kuwa ni majambazi kuuawa katika majibizano na Askari wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya.
 
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Diwani Athumani amewaambia Wandishi wa Habari Ofisini kwake kuwa Tukio hilo limetokea leo majira ya Sita Mchana katika kijiji cha Garijembe Wilaya ya Mbeya katika Barabara ya Mbeya Tukuyu.
 
Alisema Jeshi la Polisi kupata taarifa za Kinterejensia waliweka mitego mbali mbali na kufanikiwa kuwanasa watu hao wakiwa kwenye gari lenye  namba za usajili T  911 BUG aina ya Toyota Spacio ambapo baada ya kusimamishwa katika eneo hilo wakitokea Kyela kuelekea Jijini Mbeya.
Alisema baada ya kusimamishwa ghafla walianza kurusha risasi ovyo  ambapo Askari walijibu mapigo na kufanikiwa kuwajeruhi wote watano ambapo waliwafikisha katika Hospitali ya Rufaa ya Mbeya kwa ajili ya Matibabu lakini Daktari alithibitisha kuwa tayari walikuwa wamekufa.
Aliongeza kuwa baada ya kufanyiwa upekuzi walikutwa na Silaha mbili ambazo ni bunduki aina ya SMG 848628 ambapo kwenye magazine zilibaki risasi 16 na bunduki nyingine aina ya Mark III yenye namba 94695J ikiwa na risasi mbili pamoja na Koa za Shaba.
Kamanda Diwani ameongeza kuwa taarifa za Kinterejensia zilieleza kuwa majambazi hayo yalijipanga kufanya uhalifu katika maeneo ya Ushirika, Tukuyu Mjini Wilayani Rungwe pamoja na Eneo la Uyole Jijini Mbeya.
Aidha alisema majina yao wala makazi yao hayakuweza kujulikana maramoja ambapo miiliehifadhiwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mbeya na kutoa wito kwa wananchi kufika Hospitalini hapo kwa ajili ya kuwatambua ndugu zao ili wakabidhiwe kwa taratibu za mazishi.
Pia anatoa wito kwa wananchi wenye taarifa zinazohusu uhalifu kuzitoa katika mamlaka zinazohusika kwa wakati ili zifanyiwe kazi.
Jika Anda menyukai Artikel di blog ini, Silahkan klik disini untuk berlangganan gratis via email, dengan begitu Anda akan mendapat kiriman artikel setiap ada artikel yang terbit di Creating Website

0 comments:

Post a Comment

 
Support : Greyson Salufu | Chimbuko Letu Inc | Chimbuko Letu Inc
Copyright © 2011. Mbwile Media - All Rights Reserved
Template Modify by Chimbuko Letu Inc
Proudly powered by Blogger