Pages

Home » » HII NI HALI HALISI YA MLIPUKO ULIOTOKEA ARUSHA JANA

HII NI HALI HALISI YA MLIPUKO ULIOTOKEA ARUSHA JANA

 

 
DAMU ZIKITAPAKAA ENEO LA TUKIO

MAJERUHI WAKIWA CHINI

MFUKO UNAOSEMEKANA NDIYO ULIYOKUWA NA HICHO KITU KILICHOSABABISHA MLIPUKO

MAJERUHI WAKIWA HOSPITALI

 Joseph Pantaleo-Arusha, Tanzania

Uchaguzi mdogo ambao ulikuwa ufanyike leo katika kata nne za Jiji la Arusha umeahirishwa na sasa utafanyika Jumapili ijayo kutokana na bomu kuua watu watatu na kujeruhi watu wengine 60.

Katika kampeni za uchaguzi jana mtu mmoja ambaye mpaka sasa hajakamatwa alirusha bomu kwenye mkutano wa Chadema kuwaua watu hao na kujeruhi watu hao na kupelekwa kwenye Hospitali ya Mt Meru kwa matibabu zaidi.

Chama hicho jana kilikuwa kinahitimisha kampeni za uchaguzi katika Uwanja wa Soweto jijini Dar es Salaam ambako watu wengi walijitokeza kusikiliza sera za chama hicho.

Uchaguzi huo ulikuwa ufanyike kwenye kata ya; Themi, Elerai, Kaloleni na Kimandolu, lakini sasa hautafanyika tena.

Mkurugenzi wa Jiji la Arusha, Sipora Liana amesema uchaguzi huo umeahirishwa kwa kuwa wapiga kura wamepata hofu baada ya bomu hilo kulipuka kwenye mkutano wa Chadema.

Katika mkutano huo ulikuwa ikihutubiwa na Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Freeman Mbowe na viongozi wengine waandamizi wa chama hicho, lakini wakati wakikaribia kuondoka kwenye viwanja hivyo, bomu lililipuka.

Mbali na hayo Jeshi la Polisi limesema linaendelea na uchunguzi kubaini mtu au watu waliohusika katika tukio hilo.

Jika Anda menyukai Artikel di blog ini, Silahkan klik disini untuk berlangganan gratis via email, dengan begitu Anda akan mendapat kiriman artikel setiap ada artikel yang terbit di Creating Website

0 comments:

Post a Comment

 
Support : Greyson Salufu | Chimbuko Letu Inc | Chimbuko Letu Inc
Copyright © 2011. Mbwile Media - All Rights Reserved
Template Modify by Chimbuko Letu Inc
Proudly powered by Blogger