Mkuu
wa Jeshi la Polisi wa Jimbo la Bavaria na Rais wa Chuo cha Polisi
Bavaria cha Nchini Ujerumani Bw. Wolfgang Sommer akiongea na Mkuu wa
Jeshi la Polisi Nchini IGP Said Mwema wakati wakiwa katika kikao cha
pamoja na maafisa wa Polisi Makao Makuu.Bw.Sommer yupo katika ziara ya
kutembelea na kujionea mafanikio ya Jeshi la Polisi Tanzania (Picha na
Frank Geofray-Jeshi la Polisi)
Mkuu
wa Jeshi la Polisi wa Jimbo la Bavaria na Rais wa Chuo cha Polisi
Bavaria cha Nchini Ujerumani Bw. Wolfgang Sommer akimkabidhi zawadi
Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Said Mwema wakati wa ziara ya
kutembelea na kujionea mafanikio ya Jeshi la Polisi Tanzania (Picha na
Frank Geofray-Jeshi la Polisi)
Mkuu
wa Jeshi la Polisi wa Jimbo la Bavaria na Rais wa Chuo cha Polisi
Bavaria cha Nchini Ujerumani Bw. Wolfgang Sommer akiangalia jinsi ya
uendeshaji wa mafunzo katika Gym ya Polisi iliyopo katika Chuo cha
Taaluma ya Polisi Dar es Salaam (DPA) wakati wa ziara ya kutembelea na
kujionea mafanikio ya Jeshi la Polisi Tanzania (Picha na Frank
Geofray-Jeshi la Polisi)
…………………………………………………………..
Na Frank Geofray-Jeshi la Polisi
Jeshi
la Polisi nchini limefaidika kwa kiasi kikubwa na ushirikiano uliopo
kati yake na chuo cha Bavaria cha Ujerumani katika Nyanja za mafunzo,
vifaa na polisi jamii jambo ambalo limewezesha maboresho ya jeshi hilo
kuendelea vyema na kutoa huduma inayostahili kwa wananchi.
Hayo
yamebainika wakati wa ziara ya Mkuu wa Jeshi la Polisi wa Jimbo la
Bavaria na Rais wa Chuo cha Bavaria cha Nchini Ujerumani Wolfgang Sommer
alipotembelea Makao Makuu ya Jeshi la Polisi na baadhi ya vikosi vya
Jeshi hilo kujionea mafanikio ya Polisi jamii pamoja na changamoto
wanazokabiliana nazo katika utendaji wao wa kuimarisha usalama wa raia
na mali zao hapa nchini.
Akizungumza
katika ziara hiyo Kamishna wa Operesheni na Mafunzo wa Jeshi la Polisi
Paul Chagonja alisema ushirikiano baina ya chuo hicho na polisi
umesaidia kwa kiasi kikubwa katika kupata mafunzo ya jinsi ya kuimarisha
mkakati wa polisi jamii pamoja na jinsi ya kuboresha mitaala katika
vyuo vyetu vya polisi.
“Ujerumani
ni moja ya nchi zilizoendelea sana duniani hivyo na sisi kupitia
maboresho yetu tuna mambo mengi ya kujifunza ili kuendana na usasa
unaohitajika katika kuwahudumia wananchi wa Tanzania katika nyanja ya
usalama”Alisema Kamishna Chagonja.
Kwa
upande wake Mkuu wa Polisi jimbo la Bavaria na Rais wa Chuo cha Bavaria
cha Ujerumani Wolfgang Sommer alisema majeshi ya Polisi hivi sasa
duniani yanakabiliwa na changamoto nyingi kutokana na kuibuka kwa
wahalifu wenye kutumia mbinu zilizoendelea hivyo Polisi wana wajibu wa
kujifunza kwa kasi mbinu hizo.
Bw.Sommer
alisema Polisi kote duniani wapo katika maboresho hivyo kwa siku zijazo
majeshi hayo yataimarika katika kupambana na uhalifu na lengo la ziara
yake ni kujifunza mbinu zinazotumiwa na polisi wa Tanzania katuika
kukabiliana na uhalifu.
Katika
ziara hiyo alitembelea Kikosi cha matengenezo ya magari ya Polisi
ambacho kwa kiasi kikubwa kilifadhiliwa na Serikali ya Ujerumani mwaka
1994, Kikosi cha Mbwa na farasi, Chuo cha Taaluma ya Polisi (DPA),
Kikosi cha Polisi Anga pamoja na vikundi vya ulinzi shirikishi vilivyopo
katika Kanda Maalumu ya Dar es Salaam.
0 comments:
Post a Comment